Vita vya Marekani-Israel dhidi ya Iran: "Niliuza vitu vyangu nikijua nitasafiri" - Mkenya

Vita vya Marekani-Israel dhidi ya Iran: "Niliuza vitu vyangu nikijua nitasafiri" - Mkenya

Mashambulizi ya anga bado yanaendelea katika eneo la mashariki ya kati, kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Mashambulizi yanayofanywa na Marekani, Isrel na Iran yametatiza pia safari za anga katika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo Afrika mashariki, kwa wasafiri wanaopitia Dubai na maeneo mengine ya mashariki ya kati.

Sammy Luckstone Omondi ni mmoja wa wasafiri waliokwama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Moi, mjini Mombasa, Kenya amezungumza na Halima Nyanza wa BBC.