Tetesi za soka Jumatano: Aston Villa wawasilisha ofa kumsajili Mateta

Mateta

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Aston Villa wamewasilisha ofa kwa mshambuliaji wa Crystal Palace na timu ya taifa ya Ufaransa, Jean-Philippe Mateta (29), ingawa ofa hiyo iko chini sana ya thamani ambayo Palace wanaitaka.

Villa pia wako karibu kukamilisha dili la €70m (£59.8m) kumnunua mshambuliaji wa Chelsea na Senegal, Nicolas Jackson (25).

Manchester United wanafikiria kuwasiliana na Stuttgart kuhusu uwezekano wa kumsajili beki wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 20, Finn Jeltsch.

Finn Jeltsch.

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester City wanatarajiwa kuwasilisha ofa rasmi kwa Chelsea kwa ajili ya kiungo wa Argentina Enzo Fernández (25) kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Tottenham wanaweza kumnyakua winga wa Marseille na Algeria Amine Gouiri (26), ambaye pia anafuatiliwa na Napoli.

Newcastle watawasilisha ofa yao ya mwisho ya €60m (£51m) kwa mshambuliaji wa Lille na Ubelgiji Matias Fernandez-Pardo (21).

Matias Fernandez-Pardo

Chanzo cha picha, Getty Images

Leeds United na Crystal Palace wameonesha nia ya kumsajili beki wa Everton na Ireland Jake O'Brien (25).

Nottingham Forest wanafanya mazungumzo na Corinthians kuhusu kumsajili kiungo wa Brazil mwenye miaka 20, André.

Hull City wamekubaliana na Union Berlin kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani mwenye miaka 21, Ilyas Ansah. Dili hilo litagharimu zaidi ya £17.1m (€20m).