Mvuvi alivyojaribu kuwaokoa marubani wa ndege iliyopata ajali

Maelezo ya video, ''Rubani aliniambia nivunje kioo, nikakatazwa wakisema rubani anafanya mawasiliano''
Mvuvi alivyojaribu kuwaokoa marubani wa ndege iliyopata ajali

Mvuvi ambaye alikuwa mmoja wa watoa huduma wa kwanza katika eneo la ajali ya ndege iliyoua watu 19 katika Ziwa Victoria nchini Tanzania, ameeleza jinsi alivyojaribu kuwaokoa marubani waliokuwa wamekwama kwenye chumba cha rubani na jinsi alivyokaribia kupoteza maisha.

Akihojiwa akiwa hospitalini kwake katika mji wa Bukoba,Majaliwa Jackson alisema aliingiwa na hofu baada ya kuona ndege hiyo ya abiria ikija kutoka upande usiofaa, kabla ya kutumbukia Ziwa Victoria.

th