'Tarehe 27 ni kivumbi na jasho, Zanzibar hapo' - Mandonga
'Tarehe 27 ni kivumbi na jasho, Zanzibar hapo' - Mandonga
Bondia maarufu nchini Tanzania Karim Mandonga @k_mandonga hihv karibuni alisimamishwa na Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini Tanzania ili kupisha uchunguzi wa kitabibu wa afya yake baada ya kupoteza kwa Technical Knock Out (TKO) katika mapambano yake mawili ya mwisho.
Matokeo ya uchunguzi wa kitabibu yaliyofanyika yametoa majibu kuwa Mandonga hajaathirika katika maeneo yaliyofanyiwa uchunguzi na kuruhusiwa kuendelea na mapambano yake yanayokuja hivi karibuni.
Kupitia kipindi cha Dira ya Dunia kinachorushwa na YouTube channel ya BBC George Silasi Lukindo Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC) ameeleza kwa kina juu ya sababu zilizopelekea Bondia huyu kufungiwa.
Video: @frankmavura



