'Tope lilizidi, nikawaambia njooni mtoboe choo, ndio wakatoboa tukatoka'
'Tope lilizidi, nikawaambia njooni mtoboe choo, ndio wakatoboa tukatoka'
Mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia jumapili huko Manyara kaskazini mwa Tanzania, zimesababisha vifo, uharibu wa makazi na mashamba.
Asha Hassan, Mkazi wa Katesh ameiambia BBC kuwa ilibidi yeye na mjukuu wake waokolewe kupitia tundu la choo kwa usaidizi wa askari wa uokoaji.
Serikali ya Tanzania imetangaza kuwa itagharamia mazishi ya zaidi ya watu 50 ambao wamepoteza maisha yao kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo katika eneo la Katesh wilayani Hanang mkoani Manyara.
Rais Samia ambaye amekuwepo Dubai kwa ajili ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) ameamua kufupisha safari hiyo na kurejea nchini haraka iwezekanavyo ili kushughulikia kwa karibu janga hilo.



