Mamlaka za Tanzania zachunguza ugonjwa usiojulikana ulioua watu watano

Maelezo ya video,
Mamlaka za Tanzania zachunguza ugonjwa usiojulikana ulioua watu watano

Mamlaka za serikali nchini Tanzania zinachunguza ugonjwa usiojulikana ambao umesababisha vifo vya watu watano na wawili kulazwa hosptalini mkoani Kagera, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Taarifa ya Wizara ya Afya imesema watu hao saba wanasadikiwa walipata dalili za homa, kutapika, kutokwa damu maeneo mbalimbali ya mwili na figo kushindwa kufanya kazi.

Mamlaka ya mkoa wa Kagera imewataka watu kutulia wakati matokeo ya vipimo yakingojewa huku mitandao ya kijamii ikiwa na mijadala kuhusiana vifo hivyo.