Tazama: Theluji ilivyofunika baadhi ya maeneo ya Marekani
Baadhi ya maeneo ya Marekani yalifunikwa na theluji wikendi hii huku dhoruba kali ya msimu wa baridi ikikumba nchi nzima.
Wakazi katika miji ya Syracuse, New York walipambana na upepo mkali kulima njia kwenye theluji, huku hali ya baridi kali pia ikishuhudiwa huko Lowville, kaskazini ya mbali.
North Platte, katika jimbo la katikati ya magharibi la Nebraska, pia ilikumbwa na theluji.
Huduma ya Kitaifa ya Hali ya Hewa ilitoa onyo eneo hilo kwamba hali ya usafiri itazorota kutokana na theluji barabarani.
Na theluji imefunika sehemu ya uwanja wa ndege wa L&N huko Louisville, Kentucky.
Jimbo hilo ni miongoni mwa majimbo matano yaliyotangaza hali ya dharura kutokana na hali hiyo. Jimbo lingine ni lililoathiriwa ni la Missouri, ambapo barabara zilizofunikwa na the luji zilionekana huko Saint Joseph.



