'Usiwaangalie machoni': Uso kwa uso na wafungwa wa siri katika gereza-kubwa
'Usiwaangalie machoni': Uso kwa uso na wafungwa wa siri katika gereza-kubwa

Siku chache baada ya rais wa El Salvador Nayib Bukele kuchaguliwa tena, BBC imepewa fursa adimu ya kuingia katika gereza kubwa ambalo limekuwa ishara ya vita vya rais huyo dhidi ya ghasia za magenge ya uhalifu.
Serikali inasema Cecot - kituo cha kupambana na ugaidi - kinaweza kuwashikilia hadi wafungwa 40,000.
Ripoti ya hivi karibuni ya Human Rights Watch ilikosoa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.



