Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Buyenzi, kitovu cha Kiswahili na Waswahili wa Burundi
- Author, Dinah Gahamanyi
- Nafasi, Mwandishi BBC Swahili
Katikati mwa mji mkuu wa Burundi Bujumbura unapatikana mtaa maarufu sana wa Buyenzi. Umaarufu wake umetokana na kwamba eneo hili lina wakazi wenye utamaduni tofauti kabisa na ule wa wakazi wa maeneo mengine ya Burundi, kuanzia lugha, chakula mavazi na mtindo wa maisha kwa ujumla.
Eneo hili ni kitovu cha Waswahili na lugha ya kiswahili, kwa hiyo maisha yao ni ya kiswahili. Je Waswahili walifikaje Burundi nani kwanini Buyenzi ni kitovu cha Waswahili Mzee Anzuruni Hussein , mmoja wa wataalamu wa historia ya Waswahili na utamaduni wao nchini Burundi, alizungumza na mwandishi wa BBC Dinah Gahamanyi...
*Video imehaririwa na Eagan Salla