Video za uongo dhidi ya wahamiaji Tunisia zafichuliwa

Maelezo ya video, Tunisia: Video za kupotosha za kupinga wahamiaji zilizovuma mitandaoni
Video za uongo dhidi ya wahamiaji Tunisia zafichuliwa
Tunisia

Video za uwongo na za kupotosha za mitandao ya kijamii kuhusu wahamiaji kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara nchini Tunisia zimesambazwa sana huku kukiwa na wimbi la chuki dhidi ya wahamiaji.

BBC imechunguza video za mtandaoni zinazodai kuwaonyesha wahamiaji Waafrika nchini Tunisia, karibu zote zilirekodiwa kwingineko.