Mkutano wa siri uliojaribu kuzuia vurugu za muziki wa kufoka

df

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tupac Shakur aliuawa kwa kupigwa risasi mwaka 1996 akiwa na umri wa miaka 25
    • Author, Ian Youngs
    • Nafasi, BBC News World
  • Muda wa kusoma: Dakika 5

Kabla ya mvutano wa waimbaji wa kufoka foka (rapa) kutoka mashariki na magharibi katika miaka ya 1990 kuchemka na mauaji ya Tupac Shakur na Notorious BIG, mtayarishaji mashuhuri wa muziki Quincy Jones aliitisha mkutano wa siri ambapo alitoa wito wa kukomesha vurugu hizo.

Muziki wa hip-hop (kufoka foka) ulizidi kupata umaarufu kutoka mtaani hadi kwenye majukwaa makubwa katika miaka ya 90.

Quincy Jones alikuwa katika magenge na alidungwa kisu akiwa na umri wa miaka saba katika miaka ya 1930 huko Chicago, kabla ya kuwa gwiji wa muziki wa Marekani kutokana na kufanya kazi na magwiji kama Ray Charles, Frank Sinatra na Michael Jackson.

Alikuwa kiini cha mapinduzi katika muziki wa jazz, swing, soul, funk, disco na pop - lakini eneo moja la maisha yake ambalo halijazingatiwa sana hadi alipofariki wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 91 - ni nafasi yake katika hip-hop.

Pia unaweza kusoma

Jones aliheshimiwa katika pembe zote za muziki, ikiwa ni pamoja na muziki wa kufoka foka ama hip-hop.

Alifanya kazi na wasanii maarufu wa rapa katika miaka ya 80, na katika miaka ya 90 aliitambua hatari iliyoibuka katika ushindani tete kati ya lebo na nyota wa muziki huo.

Kwa hivyo aliwaleta wasanii, watendaji wakuu na wazee wa jamii ya Wamarekani weusi pamoja kwa mkutano wa siri mwaka 1995, akitumai itakuwa hatua ya mabadiliko.

Ushindani wa Muziki

K

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Notorious BIG alisajiliwa na P Diddy, kwenye lebo ya Bad Boy

Pwani ya mashariki ilikuwa ni nyumbani kwa muziki wa hip-hop. Mwaka 1992, Sean Combs - wakati huo akijulikana kama Puffy na baadaye kama P Diddy - alizindua lebo yake ya muziki ya Bad Boy huko New York na wasanii akiwemo Notorious BIG, aka Biggie Smalls.

Wakati huo huo, Los Angeles ilikuwa ikichupikia kama jiji la muzuki wa kufoka, likiongozwa na lebo tishio ya Suge Knight, Death Row Records, ambayo pia ilikuwa na wasanii Dr Dre na Tupac.

Mwaka 1994, Tupac alipigwa risasi na kujeruhiwa wakati wa uporaji kwenye ukumbi wa studio. Baadaye alidokeza kwamba rafiki yake wa zamani Biggie huenda alifahamu kuhusu shambulio hilo mapema. Kisha Biggie akatoa wimbo wa Who Shot Ya? Ambao Tupac alifikiri kuwa unamhusu.

Mkutano wa siri

SDXC

Chanzo cha picha, Madison McGaw/BFA.com/Shutterstock

Maelezo ya picha, Quincy Jones alimwomba Fab 5 Freddy kuwa msimamizi katika mkutano wa 1995
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Jones, wakati huo akiwa mmiliki wa jarida, Vibe, aliitisha mkutano 1995. Ugomvi wa mashariki-magharibi haikuwa sababu pekee ya Jones kuitisha mkutano - alikusudia pia kujadili hali ya hip-hop na kuruhusu kizazi kipya kusikia ushauri wa maisha na biashara kutoka kwa kundi la watu weusi waliofanikiwa.

Lakini taswira mbaya ya hip-hop na mivutano iliyokuwa ikiongezeka - lilikuwa jambo kubwa la kuzungumzwa.

Jones aliuambia mkutano huo: "Kitu ambacho kinaniumiza sana – ni kuhusu Tupac."

Tupac hakuwepo wakati huo - alikuwa gerezani kwa unyanyasaji wa kingono. Suge na Dre walikuwepo, pia Combs na Biggie.

Jones tayari alikuwa amepitia ugomvi wake mwenyewe na Tupac – rapa huyo alimkosoa mtayarishaji huyo katika toleo la 1993 la jarida la Source kwa kuoa wanawake weupe.

"Hatimaye tulipatana, ingawa hali ilikuwa ya mvutano hapo mwanzo," Jones alisema kwenye hafla hiyo.

"Mwishowe tulizungumza, na akasema hakuna mtu aliyezungumza naye kama hivyo hapo awali. Na nikasema, siwezi kuvumilia. Kwa sababu hatuwezi kushindwa kuzungumza."

ER

Chanzo cha picha, Amamy

Maelezo ya picha, Toleo la 1994 la jarida la Vibe lilikuwa na kichwa cha habari "Je, Tupac ni kichaa au haeleweki tu?"

Takribani wasanii na watendaji 50 mashuhuri walikuwa kwenye chumba hicho, akiwemo Public Enemy’s Chuck D wa kundi la Public Enemy, wanachama wa A Tribe Called Quest, MC Lyte, Kris Kross, Jermaine Dupri, na mtengenezaji wa filamu ya Boyz n the Hood, John Singleton.

Jones aliandika katika wasifu wake 2001: "Nilikuwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa kutofautiana kwa watu ambao hawajawahi kuwa katika chumba kimoja pamoja."

Walikuwepo pia Clarence Avant na Ahmet Ertegun, pamoja na Colin Powell, mshauri wa zamani wa usalama wa kitaifa na mkuu wa jeshi la Marekani ambaye baadaye akawa Waziri wa kwanza mweusi wa mambo ya nje.

Kwanini mkutano wa siri?

dfxc

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Quincy Jones na Colin Powell katika picha 2008

Powell alikuwa na malengo ya kisiasa - ndiyo maana mkutano huo ulifanyika kwa siri. Jones alitaka kumficha Powell asihusishwe na mambo mabaya yaliyouzingira muziki wa kufoka.

Alibadilisha ukumbi dakika za mwisho ili kuvipoteza maboya vyombo vya habari, na kuzificha kumbukumbu zote.

"Najua tutaleta mabadiliko katika mkutano huu. Labda tunaweza kubadilisha hali ya mambo." Jones alimwandikia Powell katika barua ambayo haijachapishwa iko katika Maktaba ya Chuo Kikuu cha Indianapolis.

Jones baadaye aliandika katika kitabu chake: "Baadhi ya rapa wachanga hawakumjua hata Powell ni nani na alidumisha tabia ya utulivu."

Tupac na Jones

qwe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mtoto wa Jones, Kidada alikuwa kwenye mahusiano wa kimapenzi na Tupac alipofariki

Mwaka 1993, binti wa Jones mwenye umri wa miaka 17 Rashida - ambaye ameigiza katika filamu ya The Office - aliandika barua ya hasira katika jarida la Source akimshambulia Tupac.

Tupac alipogongana na binti mmoja wa Jones, Kidada, aliomba msamaha akidhani ni Rashida. Lakini Tupac na Kidada walielewana na kuanza uhusiano.

Pia kumekuwa na madai kuwa Tupac alikuwa anapanga kuondoka Death Row na kujiunga na rekodi ya Jones.

Lakini Septemba 1996, mwaka mmoja baada ya mkutano huo, Tupac alipigwa risasi na kuuawa.

Kiongozi wa zamani wa genge, Duane "Keffe D" Davis, alishtakiwa kwa mauaji yake mwaka jana. Amekana kuhusika.

Mwaka 1997, BIG aliuawa kwa kupigwa risasi nje ya tafrija iliyoandaliwa na lebo ya Jones na jarida lake. Hakuna aliyewahi kushtakiwa.

Leo Knight yuko gerezani kwa kugonga mtu na kukimbia, na P Diddy anasubiri kesi kwa mashtaka ya ulaghai na biashara ya ngono, ambayo anakanusha.

Vurugu za miaka ya 90

sd

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Snoop Dogg, Dr Dre na Quincy Jones kwenye Tuzo za Vibe mwaka 2004

Vurugu za miaka ya 90 "hazikuwa za lazima" na zilisababishwa na watu waliotaka umaarufu na wanaohusika na magenge,” anasema msanii mkongwe, rapa na mtangazaji Fab 5 Freddy.

"Pia, ugomvi wa mashariki/magharibi ulichochewa zaidi na wivu. Ulikuwa ni moto wa jivu uliochochewa na vyombo vya habari na kusababisha Biggie na Tupac kuuawa."

Licha ya nguvu zake, Jones hakuweza kuzuia umwagaji damu. Lakini Freddy anaamini kuna la kujifunza katika mkutano huo, na unastahili kuwa na nafasi katika historia ya hip-hop.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Ambia Hirsi