Ifahamu Hospitali ya Roma inayomtibu Papa Francis

g

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Sanamu ya marehemu Papa Yohane Paulo II imesimama nje ya hospitali ya Gemelli ambako Papa Francis anapokea matibabu
Muda wa kusoma: Dakika 4

Nje ya hospitali ya Gemelli mjini Roma kuna sanamu kubwa ya mmoja wa wagonjwa wake maarufu, Papa Yohane Paulo II (John Paul II).

Imetengenezwa kwa marumaru nyeupe ya Carrara, inaonyesha papa katika miaka yake ya mwisho ya maisha yake h, akiwa ameshikilia msalaba , huku uso wake ukionekana kujaa maumivu.

Madaktari katika hospitali ya Gemelli walisaidia kuokoa maisha ya John Paul, baada ya kupigwa risasi katika jaribio la mauaji lililoshindwa katika uwanja wa Mt Peter mnamo Mei 1981.

Alifanyiwa upasuaji wa saa sita ili kuondoa risasi kutoka kwenye fumbatio lake.

Hii ni mara ya kwanza kwa Papa kutibiwa katika hospitali kubwa zaidi mjini Rome.

Miongoni mwa wagonjwa wa sasa wa hospitali hiyo ni Papa Francis, ambaye alilazwa wiki iliyopita akiwa na maambukizi ya mfumo wa kupumua. Amegunduliwa kuwa na homa ya mapafu katika mapafu yote mawili na mwishoni mwa wiki amegundulika pia ana tatizo la figo, lililo katika hatua za awali.

h
Maelezo ya picha, Marehemu Papa John Paul II, akiwa pichani wakati wa ziara yake nchini Ireland, alilazwa mara 10 katika hospitali ya Gemelli.

Katika kipindi cha miaka 25 ya upapa wake, John Paul alilazwa karibu mara 10, wakati mwingine akilazwa kwa muda mrefu. Alipata matibabu ya magonjwa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uvimbe wa tumbo, nyonga iliyovunjika na tracheotomy, wakati ugonjwa alipokuwa akiugua ugonjwa wa Parkinson uliokuwa umefikia kiwango cha juu.

Gemelli, ambayo ni hospitali ya mafundisho ya Kikatoliki, ilifunguliwa katika miaka ya 1960. Ikiwa na vitanda zaidi ya 1,500 vya wagonjwa, ni moja ya hospitali kubwa za kibinafsi barani Ulaya.

Hospitali hii iliyojengwa juu ya ardhi iliyotolewa na Papa Pius XI kwa mwanateolojia na daktari Agostino Gemelli mnamo mwaka 1934, imejulikana kama "Hospitali ya Papa."

John Paul II hata aliipa jina la utani "Vatican Three," na St Peter's Square kuwa Vatican One, na makazi ya papa huko Castel Gandolfo, Vatican Two.

Katika miaka ya 1980, Gemelli alianzisha kitengo maalum cha Papa, ambacho bado kinatumika leo.

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marehemu Papa Yohane Paulo II katika hospitali ya Gemelli

Ni nyumba ndogo iliyopo kwenye gorofa ya kumi, yenye rangi nyeupe yenye samani za bei nafuu. Ina chumba cha kulala na bafuni, kuna sebule, na kitanda pamoja na kiti cha sofa kwa ajili ya wasaidizi wake na kanisa dogo lenye mahala pa kupiga magoti kwa ajili ya ibada na msalaba mkubwa, ambapo Papa anaweza kuhudhuria au kusherehekea misa na kufanya maombi.

Njia ndefu inayoelekea kwenye chumba hicho inalindwa na polisi wa Jimbo la Italia, au Gendarmerie ya Vatican na usalama wa hospitali.

Chumba cha Papa katika hospitali hiyo kimehifadhiwa maalum kwa ajili ya mapapa, lakini wagonjwa wengine wanatibiwa kwenye gorofa moja.

Kuna veranda ambapo Papa anaweza kuonekana kuwasalimu waumini na kufanya sala ya kila wiki ya Angelus.

Mara nyingi waombolezaji hukusanyika katika uwanja nje ya hospitali ili kuombea afya ya Papa. Maua, kadi, picha na mishumaa mara nyingi huwekwa chini ya sanamu ya John Paul II.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Papa Francis awasili kwa ajili ya mkutano mkuu wa kila wiki mjini Vatican

Kwa mujibu wa tangazo rasmi, Papa Benedikto XVI hakuwahi kulazwa hospitalini wakati wa miaka 8 ya upapa wake, ingawa alitembelea hospitali hiyo wakati kaka yake alipokuwa akipokea matibabu huko mwaka 2014.

Papa Francis amekuwa akitibiwa katika hospitali ya Gemelli mara kadhaa. Mwaka 2013, alifanyiwa upasuaji kwenye utumbo wake. Alitibiwa kwa ugonjwa wa mafua mnamo Machi 2023, na alifanyiwa upasuaji wa utumbo baadaye mwaka huo.

Mara nyingi amekuwa akionekana akiishukuru timu yake ya madaktari na wafanyakazi wengine wa hospitali. Mara ya mwisho alipokuwa katiia hospitali hiyo , alimbatiza mtoto mchanga, na kushiriki chakula cha jioni cha pizza na madaktari wake, wauguzi, wasaidizi na wafanyakazi wa usalama wa Vatican.

Imehaririwa na Yusuph Mazimu