Tazama: Wakati wapiga picha wa BBC waliposhindwa kuendelea na kazi baada ya kuona jamaa zao Gaza
Tazama: Wakati wapiga picha wa BBC waliposhindwa kuendelea na kazi baada ya kuona jamaa zao Gaza
Wapiga picha wa BBC huko Gaza wamejikuta wakilazimika kuacha kupiga picha baada ya kupata mshtuko wa kuona marafiki na jamaa zao wameuawa na wengine kujeruhiwa katika shambulizi la anga la Israel.
Mwandishi wa BBC Adnan Elbursh na mpiga picha Mahmoud Al Ajrami walikuwa wakichukua picha za manusura katika Hospitali ya Al-Shifa wakati majirani zao walipoanza kuletwa miongoni mwa waliojeruhiwa.
Mamia ya miili imejaa hospitalini hapo kufuatia mashambulizi ya anga ya kilipiza kisasi shambulio la Jumamosi la Hamas ambalo liliua takriban watu 1,300 nchini Israel.
#bbcswahili #israel #gaza #hamas #Palestine



