Fahamu kilichosababisha kaa kufa kwa wingi katika fukwe za Zanzibar
Fahamu kilichosababisha kaa kufa kwa wingi katika fukwe za Zanzibar
Serikali ya Zanzibar inaendelea kuchunguza sababu zilizosababisha maelfu ya vifo vingi vya kaa chanje vilivyoshuhudiwa katika fukwe mbalimbali visiwani humo.
Serikali inasema sio mara ya kwanza tukio kama hili kutokea katika kipindi kama hiki lakini msimu huu imezua taharuki kwakuwa kaa waliokufa ni wengi zaidi kuwahi kushuhudiwa.
Ripoti ya awali inaonesha vifo vya kaa hao vinatokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
@alfredlasteck



