Wanafunzi wa sekondari Tanzania wabuni gari linalotumia nishati ya jua
Wanafunzi wa sekondari Tanzania wabuni gari linalotumia nishati ya jua

Wanafunzi sita wanaosoma katika shule ya Sekondari ya Sayansi huko Arusha nchini Tanzania wamebuni gari linalotumia nishati ya jua (sola) lenye uwezo wa kukimbia kilomita160 likiwa limebeba mzigo wa mpaka nusu tani.
Uvumbuzi huu unaotambulika na mamlaka ya elimu mkoa wa Arusha ni utekelezaji wa mafunzo kwa vitendo ambayo wamekuwa wakifundishwa shuleni hapo.
Mwandishi wa BBC alitembelea shule hii iliyopo mkoani Arusha na kutuandalia taarifa ifuatayo:
Video: Eagan Salla



