Kimbunga Hidaya: Kimbunga ni nini?
Kimbunga Hidaya: Kimbunga ni nini?
Kenya na Tanzania huenda zikakumbwa na kimbunga Hidaya kinachoarifiwa kuendelea kusogea kuelekea pwani ya bahari ya Hindi ijapokuwa kasi ya kimbunga hicho inapungua.
Zaidi ya watu 350 wamefariki dunia tangu mwanzoni mwa mwaka huu katika nchi hizo za Afrika mashariki kutokana na mvua kubwa na mafuriko, huku maelfu wengine wakilazimika kuyahama makazi yao.
Sasa kufahamu zaidi kuhusu kimbunga hiki, athari zake na vipi utakuwa salama, Elizabeth Kazibure anakufahamisha hapa zaidi.



