Tazama: Mwanafunzi alivyotembea kutoka Pakistan hadi Mecca kutimiza ndoto ya Hajj

Maelezo ya video, Kutembea kutoka Pakistan hadi Mecca kutimiza ndoto ya Hajj
Tazama: Mwanafunzi alivyotembea kutoka Pakistan hadi Mecca kutimiza ndoto ya Hajj
Usman Arshad

Mwanafunzi wa Pakistani ametembea zaidi ya kilomita 4,000 kufikia ndoto yake ya kufika Mecca kwa miguu kabla ya Hija ya mwaka huu.

Usman Arshad alianza safari yake ya miezi sita kutoka mji alikozaliwa wa Okaram kupitia Pakistan, Iran, Falme za Kiarabu na Saudi Arabia hatimaye kufika mji mtakatifu wa Mecca.