Africa Eye: Nini kilitokea kwa wafanyakazi wa nyumbani?

Maelezo ya video, Africa Eye: Nini kilitokea kwa wafanyakazi wa nyumbani?
Africa Eye: Nini kilitokea kwa wafanyakazi wa nyumbani?

Miaka mitatu iliyopita, mwandishi wa BBC Africa Eye Nancy Kacungira aliripoti kuhusu masaibu ya wafanyakazi wa nyumbani nchini Kenya.

Filamu inayojulikana kama ‘housegirls’, ilisimulia maisha yao magumu na kuonesha jinsi kuajiriwa kama mfanyakazi wa nyumbani kunavyoweza kusababisha mateso na hata unyanyasaji. Sasa Nancy amerejea na kumtafuta mmoja wao, Mercy Mwake, ili kujua maisha yake yamebadilikaje na iwapo matumaini na ndoto zake zilitimia.