Gharama za vyakula zinavyosababisha ugumu wa maisha Kenya

Zikiwa zimesalia wiki kadhaa kuelekea uchaguzi mkuu nchini Kenya, baadhi ya wananchi wa taifa hilo lenye uchumi mkubwa katika eneo la Afrika Mashariki wanaendelea kulalamikia ugumu wa maisha utokanao na kupanda kwa gharama za bidhaa muhimu kama vile unga, mafuta na bidhaa nyengine.

Hata hivyo, baadhi wana matumaini kwamba, huenda afueni ikapatikana baada ya uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 9 mwezi wa nane mwaka huu.