Je umekumbana na watu wakiuza vyeti vya uongo vya chanjo ya Uviko 19?

BBC imegundua kuna Walaghai wanaoelekeza watu kwenye Facebook kwenye tovuti zinazodai kuuza hati bandia za chanjo ya Covid kwa wale ambao hawajachanjwa.

Watu nchini Uingereza wanatakiwa kuthibitisha hali yao ya chanjo ili kufikia baadhi ya maeneo na kuepuka kujitenga baada ya kusafiri nje ya nchi.

Je umekumbana na watu wakiuza vyeti vya uongo kwa watu ambao hawajachanjwa ili kukiuka sheria.