Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ukosefu wa uelewa wa hali ya usonji nchini Tanzania
Kugongagonga vitu na kuzungumza vitu ambavyo mara nyingi ni vigumu kuvielewa na baadhi ya sifa za watu wenye tatizo la usonji, kwa Kiingereza Autism.Ukosefu wa uelewa kuhusu tatizo hili huwafanya watu kuwabagua na wazazi wengine hata uwafungia ndani watoto wao wenye tatizo la usonji ili wasionekane na umma.Ulimwengu ukiadhimisha siku ya usonji duniani leo hii na video hii ilifanywa na BBC mwaka 2016.Sammy Awami alizungumza na watu wanaohudumia watu wenye tatizo la usonji.