Mapinduzi Myanmar: Apiga picha akifanya mazoezi bila kujua jeshi linapindua serikali yake

Mwalimu wa mazoezi ambaye alikuwa anafanya mazoezi huku akijirekodi ili kujiandaa na mashindano ya kucheza, bila kujua yanayojiri nyuma yake ,picha yake hiyo ilionyesha harakati za wanajeshi katika mapinduzi ya serikali ya Myanmar.

Picha hii ya video imempatia umaarufu mkubwa ambao wala hakutarajia kuupata.