Nyota Wizkid amesema kuwa tuzo haziashirii umahiri wa msanii

Maelezo ya sauti, Nyota Wizkid amesema kuwa tuzo haziashirii umahiri wa msanii

Nyota wa muziki wa Nigeria Wizkid kwenye mazungumzo na mwanamitindo Naomi Campbell amesema kuwa upataji tuzo haumbabaishi yeye kama msanii kwani huwa zimeekwa tu na kampuni za watu . Nyota huyo wa kibao cha Joro anasema tuzo hazielezei umahiri wa msanii na yeye ananuia muziki wake kugusa watu na hiyo ndio tuzo kuliko tuzo nyingine yoyote.