Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Binti aliyekuwa akijishughulisha na biashara ya ngono abadilika na kuwa balozi wa maadili mema.
Katika miaka ya hivi karibuni biashara ya kuuza miili imekithiri miongoni mwa vijana wa kike barani Afrika, ikiwa ni njia moja wapo ya kujipatia kipato.
Nchini Tanzania Shirika la AMREF Health Afrika limeanzisha mradi maalum wa mafunzo ya mabadiliko ya tabia na kuzuia maambukizi ya VVU kwa vijana walioko kwenye makundi hatarishi.
Miongoni wa walionufaika na mradi huo ni Bi Anna Aphonse Sambaye ambaye kwa sasa ameachana na biashara hiyo na amekua akitoa elimu kwa wenzake ambao bado wanajishughulika na biashara ya kuuza miili yao.