Tangazo la kampuni ya magari ya Audi lafutiliwa mbali

Kampuni ya kutengeneza magari ya ujerumani ya Audi imeomba msamaha kwa tangazo lililoonyesha msichana mdogo akila ndizi mbele ya gari, baada ya kukosolewa vikali kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakisema picha hiyo ilikuwa na maudhui ya kingono.