Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Sensa Kenya: Fahamu umuhimu wa kuhesabiwa katika taifa lako
Nchini kenya kesho kutafanyika zoezi la kuhesabu watu yaani sensa.
Zoezi hili la watu kuhesabiwa hufanyika kila baada ya miaka kumi nchini Kenya .
Serikali hutumia shughuli hii ili kujua jinsi ya kupanga na kukadiria matumizi ya raslimali na fedha lakini pia wanasiasa hutumia idadi ya watu na maeneo walioko kutathmini azma zao za kisiasa
Lakini je wakenya wamejitayarisha vipi kwa shughuli hii?
Anne ngugi alifika kaunty ya kajiado na kuzungumza na baadhi ya wenyeji wanaoishi maeneo hayo ambapo wengi wao ni kutoka Jamii ya wamaasai ambao ni watu wa kuhama hama