Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Koffi Olomide awaomba msamaha akina mama Afrika
Koffi Olomide mwimbaji maarufu barani Afrika na Ulaya ametoa wimbo mpya ambao ni wa kuombea msamaha akina mama wote Afrika baada ya kumpiga kwa kiwiko mnenguaji wake mwaka jana akiwa nchini Kenya.Tukio hilo lilisababisha kuzuiliwa kwa mfululizo wa matamasha yake nchini humo na baadala yake alikamatwa na serikali ya Kenya na kufurushwa na akarejea nchini Congo.