Kilio, aibu na shangwe ndio sura iliyokumba nusu fainali ya kwanza Brazil
Maelezo ya picha, Bao la kwanza la Ujerumani lilipokewa kwa vifijo na nderemo na mashabiki waliokuwa wamejaa pomoni kushuhudia timu yao ikimenyena na mabingwa mara sita wa kombe la dunia Brazil
Maelezo ya picha, Mechi hii ilikua ya kwanza ya nusu fainali katika kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil
Maelezo ya picha, Wengi wamesema wachezaji wa Ujerumani walikuwa 'balaa' yaani walikuwa wakali katika mechi hiyo
Maelezo ya picha, Kipa wa Ujerumani hakuwa na chochote cha kufanya kwani hali ilikuwa ngumu kweli.
Maelezo ya picha, Ilikuwa sherehe kila pembe ya dunia kutoka kwa mashabiki wa Ujerumani na hata nyumbani baada ya timu yao kuingiza mabao matano katika dakika za kwanza 29 za mechi hiyo
Maelezo ya picha, Mabao yaliendelea kuingizwa hadi yakafika saba mwishoni mwa mechi. Brazil hata hivyo walikomboa bao moja la kupanguzia machozi, ila halikutosha kuondoa aibu waliyoipata katika mchuano huu ambao umewaacha wengi vinywa wazi
Maelezo ya picha, Mashabiki wa Brazil walikuwa wanajionea giza uwanjani magoli yakiingizwa na Ujerumai kutoka pembe zote za uwanja
Maelezo ya picha, Ujerumani sasa watajiandaa kumenyana na mshindi wa mechi kati ya Uholanzi na Argentina Brazil itasalia kupigania nafasi ya tatu
Maelezo ya picha, Huzuni ulitanda Brazil na kote duniani kwa mashabiki wa Brazil
Maelezo ya picha, Lakini nahodha wa muda wa Brazil David Luiz amewataka mashabiki wa timu hiyo kote duniani kuwasamehe wachezaji waliokuwa uwanjani Selecao,walipoadhibiwa kichapo cha mabao 7-1 na Ujerumani katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la dunia huko Brazil.
Maelezo ya picha, Kwa sasa hadi fainali za kombe la dunia ni sherehe kote kote nchini Ujerumani