Africa Eye: Unyanyasaji majumbani wakati wa janga la corona Kenya
Wakati janga la Covid-19 lilipotokea, ripoti za unyanyasaji wa nyumbani zilienea ulimwenguni kote. Nchini Kenya, kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo hivyo - na wanaharakati wanasema wengi hawaripotiwi kamwe. Tom Odula anaripoti kutoka Nairobi, kwa timu ya BBC ya uchunguzi wa Africa Eye… na onyo, baadhi ya watazamaji wanaweza kupata ripoti yake kuwa ya kufadhaisha.