Kipa wa Chelsea Edouard Mendy
Edouard Mendy amevutia wengi katika uwanja wa Stamford Bridge tangu aliposajiliwa na Chelsea kutoka klabu ya Ufaransa ya Rennes mwezi Septemba 2020 na ni miongoni mwa kikosi cha klabu hiyo kilichoshinda kombe la klabu bingwa Ulaya mwezi Mei.
Alifanikiwa kuweka rekodi ya mechi tisa bila kufungwa kabla ya kupata ushindi wa taji hilo katika msimu wake wa kwanza . Mendy pia aliweka historia kwa kuwa kipa wa kwanza Mwafrika kushiriki katika mechi za fainali za klabu bingwa Ulaya na mara ya kwanza katika michuano hiyo tangu kipa wa Zimbabwe Bruce Grobbelaar alipocheza katika fainali ya kombe la Ulaya akiichezea Liverpool.
Mendy alicheza mechi 19 bila kufungwa msimu uliopita katika michunao ya klabu bingwa ligi ya uingereza kabla ya kushinda taji la Uefa la kipa bora msimu wa 2020-21.
Mshindi huyo wa Uefa supercup pia ameteuliwa kuwania taji la Fifa la kipa bora 2021, lakini mtu aliyeibuka katika nafasi ya pili katika kombe la FA mwezi Mei , hivi majuzi alishindwa kushinda taji Yshind Trophy kutoka Ufaransa kwa kuwa kipa bora