Wapanda miti ya matunda makaburini ili kutunza mazingira
Familia ya marehemu Leonard Massawe inaendeleza ndoto yake ya kupanda miti ya matunda makabarini ili kutunza mazingira
Mwanaharakati huyo wa mazingira alihamasisha upandaji miti maeneo mbalimbali mkoani Kilimanjaro na aliamini watu wakiendelea kujenga makaburi kama wengi wanavyofanya sasa watamaliza mashamba yao.
Mwandishi wa BBC Yusuph Mazimu alizingumza na mke wake alipomtembelea nyumbani kwake kijiji cha kifuni mkoani Kilimanjaro