Jiwe la ambergris lililopatikana ndani ya nyangumi lawaondolea umasikini wavuvi Yemen

Maelezo ya video, Jiwe la ambergris lililopatikana ndani ya nyangumi lawaondolea umasikini wavuvi Yemen

Kundi moja la wavuvi nchini Yemen lilipata mabaki ya nyangumi aliyekuwa akiolea katika bahari ya Ghuba la Aden. Madini adimu waliyogundua ndani ya tumbo lake yamewaondolea umaskini na kusaidia wengine katika kijiji chao. Ambergris, iliyotengenezwa ndani ya matumbo ya nyangumi ni madini muhimu yanayotumika katika kutengeneza manukato na kuhifadhi harufu. Filamu na Eloise Alanna, Suaad Al-Salahi na Adnan Ameen Al-Haaj