Champions League: Samatta apangiwa mabingwa Liverpool

Mbwana Samatta

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mbwana Samatta anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kucheza Champions League

Makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yameshapangwa na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji inayochezewa na Mtanzania Mbwana Samatta wataminyana na bingwa mtetezi Liverpool kutoka England.

Siku 89 zilizopita, Liverpool ilinyanyua ndoo hiyo na hii leo safari ya kulitetea kombe lao imeanza kupata uhai.

Samatta ambaye ni mshambuliaji bora nchini Ubelgiji atakuwa na kibarua kigumu cha kumpita beki bora wa Ulaya Vigil van Dijk.

Makundi kamili ni kama yalivyo hapo chini:

Kundi A

  • Paris Saint-Germain
  • Real Madrid
  • Club Brugge
  • Galatasaray

Kundi B

  • Bayern Munich
  • Tottenham
  • Olympiakos
  • Red Star

Kundi C

  • Man City
  • Shakhtar
  • GNK Dinamo
  • Atalanta

Kundi D

  • Juventus
  • Atletico Madrid
  • Bayer Leverkusen
  • Lokomotiv Moskva

Kundi E

  • Liverpool
  • Napoli
  • Salzburg
  • KRC Genk
kOMBE LA uLAYA

Kundi F

  • Barcelona
  • Borrusia Dortmund
  • Inter Milan
  • Slavia Praha

Kundi G

  • Zenit
  • Benfica
  • Lyon
  • RB Liepzig

Kundi H

  • Chelsea
  • Ajax
  • Valencia
  • Lille