Washindi na washindwa wa michezo ya Jumuiya na madola Gold Coast

Wenyeji wa mashindano huyo huko Gold Coast - Australia wanaongoza na dhahabu 39, Uganda ikiwa katika nafasi ya 12, Kenya ya 21 na Mauritius ya 23.

Rwanda voliboli
Maelezo ya picha, Timu ya Rwanda ya voliboli ya ufukweni jana imeshinda mechi yake ya kwanza dhidi ya Singapore.
Fathiya Pazi mcheza tenisi ya meza Tanzania
Maelezo ya picha, Fathiya Pazi amemshinda mpinzani wake wa Tuvalu 4-0 na hivyo kuwa mchezaji pekee wa Afrika Mashariki kuibuka mshindi mechi za tenisi ya meza kufikia sasa
Akishinda mechi yake ya pili leo jioni, Fathiya Pazi ataingia awamu ya mtoano
Maelezo ya picha, Akishinda mechi yake ya pili leo jioni ya tenisi ya mezani, Fathiya Pazi ataingia awamu ya mtoano.
Bondia wa Uganda Juma Miiro
Maelezo ya picha, Bondia wa Uganda Juma Miiro amemshinda Shafi Bakari wa Kenya uzani wa light-fly na kufuzu nusu-fainali hivyo basi kuihakikishia Uganda medali ulingoni.
Bondia Shafi Bakari wa Kenya
Maelezo ya picha, Shafi Bakari wa Kenya aliibusu sakafu raundi ya pili na kuhesabiwa hadi nane. Matumaini ya Kenya sasa yako kwa Christine Ongare uzani wa fly anayecheza kesho na bondia wa Sri Lanka.
Masoud Mtalaso wa Tanzania (kushoto) na Halima Nambozo wa Uganda
Maelezo ya picha, Masoud Mtalaso wa Tanzania (kushoto) na Halima Nambozo wa Uganda wote wamepoteza mechi zao za kwanza katika mchezo wa tenisi ya mezani.