Sauti Sol waomba mfumo wa elimu Kenya kubadilishwa

Wanamuziki maarufu nchini Kenya, Sauti Sol wanaamini tatizo linaloendelea nchini Kenya ambapo shule zimekuwa zikichomwa linaweza kwisha endapo mfumo wa elimu utabadilika na kuanza kuweka mkazo katika masuala mengine ya maisha badala ya kusisitiza ufaulu wa mitihani pekee.Sauti Sol ambao shule yao ya zamani ni moja ya zilizowahi kuchomwa moto na kusababisha kifo, wamefanya mazungumzo na mwandishi wetu Arnold Kayanda na kueleza adhima yao namna wanavyo shiriki kuzuia matukio hayo.