Kondakta wa muziki wa klasiko Tanzania
Unaufahamu au umepata kuusikia muziki wa miondoko ya klasiko? Aina hii ya muziki si maarufu sana miongoni mwa Waafrika wengi kama ilivyo katika nchi za Kimagharibi.
Mbele yao hukaa muuongozaji ajulikanaye kama kondakta. Nchini Tanzania, kuna kondakta mmoja tu wa muziki huu, anaitwa Hakima Raymond.
Hivi karibuni amefanya tamasha la kusisimua jijini Dar es Salaam, na mwandishi wetu Sammy Awami alihudhuria tamasha hilo mwanzo akitaka kujua ilikuwaje akajiunga na muziki huo?