Joh Nzenze bado anatamba kimuuziki
John Nzenze mwenye umri wa miaka 76 ni mwanamuziki mkongwe ambaye bado nyimbo zake zinatamba Afrika mashariki huku akishiriki katika matamasha ya kimataifa.
Nzenze alirekodi album yake ya kwanza mnamo mwaka wa 1962 na alishirikiana na wakongwe wa muziki kama vile marehemu Daudi Kabaka na David Amunga miongoni mwa Wengine.
Baadhi ya nyimbo zake zilizovuma ni pamoja na ile ya Angelike na Amina. Paul Nabiswa alizungumza naye nyumbani kwake huko Kaimosi, magharibi mwa Kenya.