Fahali avutishwa bangi kupigana
Fahali aliyepewa jina la Messi alimcharaza mpinzani wake Simba na kudhirihisha ubabe wake.
Fahali huyo alipewa jina hilo la utani la Messi kuonyesha umarufu wake wa kupigana kama mchezaji hodari wa kandanda wa klabu ya Barcelona Lionel Messi.
Pigano hilo la mafahali lilifanyika katika uwanja wa Bukhungu kaunti ya Kakamega eneo la magharibi nchini Kenya wikendi iliyopita.
Katika pambano hilo fahali mmoja alivutishwa bangi ili ashinde pambano
Mwandishi wa Nairobi John Nene alihudhuria pambano hilo na hii hapa ni taarifa yake.