Majengo ya Iran yenye mvuto

Mwanafunzi Mohammad Domiri ana umri wa miaka 23 na picha hizi alizipiga ndani ya majengo ya Iran

Mpiga picha mwenye umri wa miaka 23 na mwanafunzi wa sayansi, kutoka katika chuo kikuu cha Nothern Iran, Mohammad Domiri, amekuwa akipiga picha hizi zenye kuonyesha rangi mbali mbali na miundo ya kupendeza katika sehemu za maombi Mashariki ya kati.
Maelezo ya picha, Mpiga picha mwenye umri wa miaka 23 na mwanafunzi wa sayansi, kutoka katika chuo kikuu cha Nothern Iran, Mohammad Domiri, amekuwa akipiga picha hizi zenye kuonyesha rangi mbali mbali na miundo ya kupendeza katika sehemu za maombi Mashariki ya kati.
Anapokuwa ndani ya jengo lolote, Mohammad Domiri, hulenga zaidi madirisha yenye rangi na minara ya jengo.
Maelezo ya picha, Anapokuwa ndani ya jengo lolote, Mohammad Domiri, hulenga zaidi madirisha yenye rangi na minara ya jengo.
''Nyingi ya picha zangu, huonyesha upana wote wa picha, katika jengo moja,''anasema mpiga picha. Hii ni sehemu ya juu zaidi ya msikiti wa Vakil
Maelezo ya picha, ''Nyingi ya picha zangu, huonyesha upana wote wa picha, katika jengo moja,''anasema mpiga picha. Hii ni sehemu ya juu zaidi ya msikiti wa Vakil
Mohammad Domiri pia hutumia teknolojia ya hali ya juu kupiga picha zake, ili kuleta sura nzuri kwa picha zake. Picha hii ni ya msikiti wa Seyyed katika eneo la Isfahan
Maelezo ya picha, Mohammad Domiri pia hutumia teknolojia ya hali ya juu kupiga picha zake, ili kuleta sura nzuri kwa picha zake. Picha hii ni ya msikiti wa Seyyed katika eneo la Isfahan
Kwa sababu ya masharti mengi, kuhusu sehemu anakoweza kuweka vifaa vyake vya kupigia picha, huwa ni vigumu sana kupiga picha ndani ya majengo makubwa. Hii ni picha ya dari ya jumba la muziki katika kasri la Alqapu eneo la Isfahan
Maelezo ya picha, Kwa sababu ya masharti mengi, kuhusu sehemu anakoweza kuweka vifaa vyake vya kupigia picha, huwa ni vigumu sana kupiga picha ndani ya majengo makubwa. Hii ni picha ya dari ya jumba la muziki katika kasri la Alqapu eneo la Isfahan
''Nchini Iran tuna maeneo mengi ya kihistoria, lakini baadhi ya majengo makubwa ni maeneo ya kufanyia maombi kama msikiti. Tuna msikiti mkubwa katika kila mji na majengo mengi ya kihistoria yenye michoro mizuri,'' asema Mohammad Domiri.
Maelezo ya picha, ''Nchini Iran tuna maeneo mengi ya kihistoria, lakini baadhi ya majengo makubwa ni maeneo ya kufanyia maombi kama msikiti. Tuna msikiti mkubwa katika kila mji na majengo mengi ya kihistoria yenye michoro mizuri,'' asema Mohammad Domiri.
Labda baadhi ya maeneo ya kihistoria, hayatakuwepo tena katika miaka 20 ijayo. Ninapopiga picha hizi mimi hufikiria kuhusu ambavyo itahifadhiwa katika siku za usoni.
Maelezo ya picha, Labda baadhi ya maeneo ya kihistoria, hayatakuwepo tena katika miaka 20 ijayo. Ninapopiga picha hizi mimi hufikiria kuhusu ambavyo itahifadhiwa katika siku za usoni.
Mohammad Domiri ametumia masaa mengi, akifanya utafiti na wataalamu wa ujenzi, na yeye hupenda kutumia mifumo na vifaa tofauti tofauti katika kupiga picha zake.
Maelezo ya picha, Mohammad Domiri ametumia masaa mengi, akifanya utafiti na wataalamu wa ujenzi, na yeye hupenda kutumia mifumo na vifaa tofauti tofauti katika kupiga picha zake.
''Napenda, ambavyo wanaruhusu mwangaza kuingia ndani ya jumba hili,'' (Vakil Bathhouse -Shiraz)
Maelezo ya picha, ''Napenda, ambavyo wanaruhusu mwangaza kuingia ndani ya jumba hili,'' (Vakil Bathhouse -Shiraz)
Kazi yake yote ambayo hutokana na yeye mwenyewe kupenda rangi na picha hizi zote zilipigwa nchini Iran.
Maelezo ya picha, Kazi yake yote ambayo hutokana na yeye mwenyewe kupenda rangi na picha hizi zote zilipigwa nchini Iran.