Ulemavu si sababu ya kubweteka

Pamoja na changamoto ya ulemavu, walemavu wana nafasi ya kujishughulisha kujipatia riziki

Walemavu wamekuwa katika hali ya kukosa msaada hasa wakikabiliwa na changamoto ya kunyanyapaliwa na jamii inayowazunguka, hali inayowafanya kuwa ombaomba.Picha hizi zimepigwa na Mwandishi wa BBC Leonard Mubali
Maelezo ya picha, Walemavu wamekuwa katika hali ya kukosa msaada hasa wakikabiliwa na changamoto ya kunyanyapaliwa na jamii inayowazunguka, hali inayowafanya kuwa ombaomba.Picha hizi zimepigwa na Mwandishi wa BBC Leonard Mubali
Lakini hali ni tofauti kwa Philipo Paul anayeishi Tabora magharibi mwa Tanzania ameona ulemavu wake wa macho si tija katika kuendesha maisha yake ya kila siku
Maelezo ya picha, Lakini hali ni tofauti kwa Philipo Paul anayeishi Tabora magharibi mwa Tanzania ameona ulemavu wake wa macho si tija katika kuendesha maisha yake ya kila siku
Pamoja na ulemavu wa kutoona Philipo anafanya biashara ya kuuza machungwa na kujipatia kipato chake ,anasema haungi mkono tabia ya kuombaomba
Maelezo ya picha, Pamoja na ulemavu wa kutoona Philipo anafanya biashara ya kuuza machungwa na kujipatia kipato chake ,anasema haungi mkono tabia ya kuombaomba
Philipo huzitambua pesa kwa kuzipapasa sarafu, kisha hujua sarafu ya mia moja na mia mbili, hata hivyo akikabidhiwa noti huelezwa tu na mnunuzi lakini je wanauaminifu wa kutosha?
Maelezo ya picha, Philipo huzitambua pesa kwa kuzipapasa sarafu, kisha hujua sarafu ya mia moja na mia mbili, hata hivyo akikabidhiwa noti huelezwa tu na mnunuzi lakini je wanauaminifu wa kutosha?