Je Ilikuwa ajali au ndege ilidunguliwa?

Wachunguzi waruhusiwa kuingia eneo la mkasa wa ndege ya Malaysia kubaini chanzo cha kuanguka kwa ndege ya Malaysia

Maafisa nchini Ukraine wanasema kuwa ndege ya abiria iliyoanguka nchini humo ilidunguliwa katika eneo la mashariki mwa taifa hilo ambako waasi wanaoiunga mkono Urusi wamekuwa wakipigana na vikosi vya serikali.
Maelezo ya picha, Maafisa nchini Ukraine wanasema kuwa ndege ya abiria iliyoanguka nchini humo ilidunguliwa katika eneo la mashariki mwa taifa hilo ambako waasi wanaoiunga mkono Urusi wamekuwa wakipigana na vikosi vya serikali.
Ndege hiyo ilikuwa na abiria 298 ikiwemo watoto wadogo watatu. Ilikuwa safarini kutoka Amsterdam kuelekea Kuala Lumpur
Maelezo ya picha, Ndege hiyo ilikuwa na abiria 298 ikiwemo watoto wadogo watatu. Ilikuwa safarini kutoka Amsterdam kuelekea Kuala Lumpur
Mabaki ya ndege ilitapakaa kila sehemu katika ajali hiyo iliyotokea Alhamisi usiku
Maelezo ya picha, Mabaki ya ndege ilitapakaa kila sehemu katika ajali hiyo iliyotokea Alhamisi usiku
Haya ni baadhi ya masalia ya ndege hiyo ya muundo wa jet karibu na kijiji cha Grabovo, kinachodhibitiwa na waasi wanaotaka kujitenga na Ukraine
Maelezo ya picha, Haya ni baadhi ya masalia ya ndege hiyo ya muundo wa jet karibu na kijiji cha Grabovo, kinachodhibitiwa na waasi wanaotaka kujitenga na Ukraine
Ndege hiyo nambari MH17 ilikua inakaribia kuingia anga ya Urusi mawasiliano yalipokatizwa.
Maelezo ya picha, Ndege hiyo nambari MH17 ilikua inakaribia kuingia anga ya Urusi mawasiliano yalipokatizwa.
Rais wa Ukraine Petrop Poroshenko alielezea tukio hilo kuwa ni tendo la kigaidi huku waasi wakikanusha kuidungua. .
Maelezo ya picha, Rais wa Ukraine Petrop Poroshenko alielezea tukio hilo kuwa ni tendo la kigaidi huku waasi wakikanusha kuidungua. .
Inaaminiwa waasi wanaotaka kujitenga na Ukraine walizidungua ndege mbili za jeshi la Ukraine katika eneo hilo hivi karibuni.
Maelezo ya picha, Inaaminiwa waasi wanaotaka kujitenga na Ukraine walizidungua ndege mbili za jeshi la Ukraine katika eneo hilo hivi karibuni.