Ebola ni janga Afrika Magharibi

Hapa ndipo homa kali ya Ebola ilipowafikisha wakazi wa mataifa ya Afrika Magharibi

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetaka "hatua za dharura" zichukuliwe ili kudhibiti kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola Africa magharibi, ambao umewauwa zaidi ya watu 400. Ugonjwa huu ndio mkubwa zaidi duniani kuzuka kutokana na visa vyake, vifo na kusambaa katika maeneo.
Maelezo ya picha, Shirika la Afya Duniani (WHO) limetaka "hatua za dharura" zichukuliwe ili kudhibiti kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola Africa magharibi, ambao umewauwa zaidi ya watu 400. Ugonjwa huu ndio mkubwa zaidi duniani kuzuka kutokana na visa vyake, vifo na kusambaa katika maeneo.
Kumekuwepo na visa visivyopungua 600 nchini Guinea - ambapo ugonjwa huo ulianza kuzuka miezi minne iliyopita mjini Guekedou, ambao ulikuwa kituo kikubwa cha biashara, kilichowavutia wauzaji na wanunuzi kutoka mataifa kadhaa.
Maelezo ya picha, Kumekuwepo na visa visivyopungua 600 nchini Guinea - ambapo ugonjwa huo ulianza kuzuka miezi minne iliyopita mjini Guekedou, ambao ulikuwa kituo kikubwa cha biashara, kilichowavutia wauzaji na wanunuzi kutoka mataifa kadhaa.
Shirika la misaada la Medecins Sans Frontieres (MSF) tayari limeonya kuwa kusambaa kwa ebola hakuwezi kudhibitiwa. Shirika hilo lina wafanyikazi 300 wa kimataifa na vile vile wa kitaifa wanaofanya kazi nchini Guinea, Sierra Leone pamoja na Liberia, ambako ugonjwa huo unaenea kwa kasi. Mataifa mengine yako macho iwapo ugonjwa huo utasambaa Zaidi.
Maelezo ya picha, Shirika la misaada la Medecins Sans Frontieres (MSF) tayari limeonya kuwa kusambaa kwa ebola hakuwezi kudhibitiwa. Shirika hilo lina wafanyikazi 300 wa kimataifa na vile vile wa kitaifa wanaofanya kazi nchini Guinea, Sierra Leone pamoja na Liberia, ambako ugonjwa huo unaenea kwa kasi. Mataifa mengine yako macho iwapo ugonjwa huo utasambaa Zaidi.
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani, Ebola ni ugonjwa unaosababishwa na virusi na ambao dalili zake za mwanzo huweza kuwa kushikwa na homa, kuwa dhaifu, kuumwa na misuli na kuumwa na koo. Na huo ni mwanzo tu: kile kinachofuata ni kutapika, kuendesha na -wakati mwingine- kuvuja damu.
Maelezo ya picha, Kwa mujibu wa shirika la afya duniani, Ebola ni ugonjwa unaosababishwa na virusi na ambao dalili zake za mwanzo huweza kuwa kushikwa na homa, kuwa dhaifu, kuumwa na misuli na kuumwa na koo. Na huo ni mwanzo tu: kile kinachofuata ni kutapika, kuendesha na -wakati mwingine- kuvuja damu.
Virusi hivyo huenea kwa haraka sana, na hadi sasa hakuna dawa inayotambulika kuweza kuvitibu, kwa hivyo wanaotoa huduma za matibabu huvalia mavazi yanayowakinga kutokana na kuambukizwa kwa ugonjwa huo. Kulingana na uzito wa athari za ugonjwa huo, hadi kufikia asilimia 90 ya walioambukizwa huaga dunia. Anayehakikisha usafi anawakaribia wagonjwa wanaosubiri matokeo baada ya kupimwa damu.
Maelezo ya picha, Virusi hivyo huenea kwa haraka sana, na hadi sasa hakuna dawa inayotambulika kuweza kuvitibu, kwa hivyo wanaotoa huduma za matibabu huvalia mavazi yanayowakinga kutokana na kuambukizwa kwa ugonjwa huo. Kulingana na uzito wa athari za ugonjwa huo, hadi kufikia asilimia 90 ya walioambukizwa huaga dunia. Anayehakikisha usafi anawakaribia wagonjwa wanaosubiri matokeo baada ya kupimwa damu.
Vipimo vya maabara vitaonyesha kwa saa kadhaa iwapo sampuli ya damu inayopimwa ina virusi vya Ebola au la.
Maelezo ya picha, Vipimo vya maabara vitaonyesha kwa saa kadhaa iwapo sampuli ya damu inayopimwa ina virusi vya Ebola au la.
Baada ya kukumbana na virusi hivyo katika sehemu iliyotengwa, mavazi na viatu husafishwa kwa Chlorine.
Maelezo ya picha, Baada ya kukumbana na virusi hivyo katika sehemu iliyotengwa, mavazi na viatu husafishwa kwa Chlorine.
Kando na kutoa huduma za kliniki, kikundi hicho hutoa hamasisho kuhusu ugonjwa huo. Hapa Touloubengo, familia tano ambazo nyumba zao zilikuwa zimesafishwa siku kadhaa zilizopita kutokana na kuaga dunia kwa mmoja wao wanakabidhiwa magodoro.
Maelezo ya picha, Kando na kutoa huduma za kliniki, kikundi hicho hutoa hamasisho kuhusu ugonjwa huo. Hapa Touloubengo, familia tano ambazo nyumba zao zilikuwa zimesafishwa siku kadhaa zilizopita kutokana na kuaga dunia kwa mmoja wao wanakabidhiwa magodoro.
Sio kila mtu aliye salama. Hapa familia ya Kinda Marie Kamano, akiwemo dadake (katikati), pamoja na wanajamii wengine wanahuzunika katika mazishi yake karibu na nyumba yake.
Maelezo ya picha, Sio kila mtu aliye salama. Hapa familia ya Kinda Marie Kamano, akiwemo dadake (katikati), pamoja na wanajamii wengine wanahuzunika katika mazishi yake karibu na nyumba yake.
Sio kila mtu yuko salama. Hapa familia ya Kinda Marie Kamano, akiwemo dadake (katikati), pamoja na wanajamii wengine wanahuzunika katika mazishi yake karibu na nyumba yake.
Maelezo ya picha, Sio kila mtu yuko salama. Hapa familia ya Kinda Marie Kamano, akiwemo dadake (katikati), pamoja na wanajamii wengine wanahuzunika katika mazishi yake karibu na nyumba yake.
Takriban watu 600 wamefariki kutokana na homa ya Ebola Afrika Magharibi
Maelezo ya picha, Takriban watu 600 wamefariki kutokana na homa ya Ebola Afrika Magharibi