Israel Gaza: Netanyahu anafanya 'kosa', asema Biden

Rais wa Marekani Joe Biden amesema anaamini kuwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anafanya "kosa" katika kulishughulikia suala la mzozo wa Gaza.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Zambia yafichua kundi 'la kisasa' la uhalifu wa mtandaoni la China

    Huduma ya Golden Top Support Services iliajiri "Wazambia wenye umri wa kati ya miaka 20 na 25, ilisema DEC.

    Chanzo cha picha, Drug Enforcement Commission

    Shirika la kisasa la utapeli kwenye mtandao limefichuliwa nchini Zambia, na kusababisha watu 77 kukamatwa, wakiwemo raia 22 wa China.

    Yalikuwa "mafanikio makubwa katika vita dhidi ya uhalifu wa mtandao", mamlaka ilisema baada ya uvamizi dhidi ya shirika linalomilikiwa na Wachina.

    Kampuni hiyo iliwaajiri Wazambia ambao waliamini wangekuwa mawakala wa kituo cha simu. Miongoni mwa vifaa vilivyokamatwa ni vifaa vinavyowaruhusu wapigaji kuficha mahali walipo na maelfu ya Sim kadi.

    Kampuni ya Golden Top Support Services, iliyohushwa na uvamizi huo, haijatoa maoni yoyote kuhusu madai hayo.

    Uvamizi huo katika majengo yake, yaliyoko Roma, kitongoji cha mji mkuu, Lusaka, uliongozwa na Tume ya Kupambana na Dawa za Kulevya (DEC) na pia ulihusisha polisi, idara ya uhamiaji na kitengo cha kupambana na ugaidi.

    Hatua hiyo Ilikuja baada ya miezi kadhaa ya kukusanya taarifa za kijasusi na mashirika kufuatia ongezeko la kutisha la visa vya ulaghai kwenye mtandao nchini Zambia, mkurugenzi mkuu wa DEC Nason Banda alisema baada ya uvamizi huo wa Jumanne.

  2. Wapalestina waomboleza 14 waliouawa katika shambulizi usiku

    Athari za shambulizi

    Chanzo cha picha, EPA

    Wapalestina wamekusanyika kuomboleza vifo vya raia 14 waliouawa katika shambulizi linalodaiwa kufanywa na Israel jana usiku.

    Kulingana na shirika la habari la AFP, nyumba ya familia ilipigwa katika shambulio hilo.

    Shirika rasmi la habari la Palestina Wafa linaripoti kuwa wengi wa waliopoteza maisha walikuwa wanawake na watoto.

    Picha zinaonesha watu waliokusanyika katika hospitali ya karibu ya al-Aqsa Martyrs huko Deir el-Balah wakiomboleza wafu.

  3. Luke Fleurs: Sita wakamatwa kwa mauaji ya mwanasoka wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini

    Beki Luke Fleurs alijiunga na Kaizer Chiefs Oktoba mwaka jana

    Chanzo cha picha, Kaizer Chiefs

    Watu sita wamekamatwa kuhusiana na mauaji ya mwanasoka wa Afrika Kusini Luke Fleurs.

    Nyota huyo wa Kaizer Chiefs mwenye umri wa miaka 24 alipigwa risasi na kufa katika tukio la utekaji nyara katika kituo cha mafuta mjini Johannesburg wiki iliyopita.

    Katika taarifa, polisi walisema kuwa washukiwa hao sita walikamatwa huko Soweto Jumatano asubuhi.

    Polisi wanasema wanaamini "washukiwa hao ni sehemu ya kundi ambalo linahusika na utekaji nyara" katika jimbo la Gauteng.

    Wachunguzi bado wanawasaka washukiwa zaidi. Maafisa walisema walipata gari la mwanasoka huyo, ambalo lilikuwa limeibiwa baadhi ya vifaa siku ya Jumatatu.

    Bw Fleurs alikuwa akisubiri kuhudumiwa katika kituo cha mafuta alipofikiwa na watu wasiojulikana wenye silaha, ambao wakamwamuru ashuke nje ya gari, mamlaka zilisema.

  4. Shinikizo la Biden kwa Israeli halitoshi, wasema maafisa wa Marekani

    Biden

    Chanzo cha picha, Reuters

    Shinikizo la Rais wa Marekani Joe Biden kwa Israel baada ya shambulio baya la wiki jana dhidi ya wafanyakazi wa misaada halikufika mbali na litashindwa kukomesha mzozo wa kibinadamu huko Gaza, kwa mujibu wa maafisa wa sasa na wa zamani wa Marekani ambao wamezungumza na BBC.

    Walisema upinzani wa ndani serikalini unakua na kutaka hatua kali zaidi zichukuliwe katika uhamishaji wa silaha.

    Israel ilisema itafungua njia mpya za msaada baada ya Biden kutishia kutathmini upya sera kufuatia mashambulizi ya Israel yaliyowaua wafanyakazi saba wa shirika la chakula la World Central Kitchen (WCK), akiwemo raia wa Marekani na Canada.

    Annelle Sheline, afisa anayefanya kazi katika haki za binadamu ambaye alijiondoa katika idara ya serikali kwa maandamano wiki mbili zilizopita. Alisema Ikulu ya Marekani "ingeweza kufanya hivyo miezi kadhaa iliyopita na kuzuia njaa kaskazini mwa Gaza".

    Uhusiano wa Marekani na Israel kwa sasa unakabiliwa na mzozo mkubwa zaidi katika miongo kadhaa, baada ya mazungumzo ya simu ya Biden na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wiki iliyopita.

  5. Uhispania ipo 'tayari kulitambua taifa la Palestina' - Waziri Mkuu

    Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sánchez akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari huko Jordan tarehe 2 Aprili

    Chanzo cha picha, Reuters

    Waziri Mkuu Pedro Sánchez anasema Uhispania iko tayari kulitambua taifa la Palestina na kwamba kutambuliwa itakuwa hatua ya kusuluhisha mzozo wa Mashariki ya Kati.

    Katika hotuba yake kwa Bunge la Uhispania leo asubuhi, anasema ni "kwa maslahi ya kijiografia ya Ulaya" anapojaribu kupata uungwaji mkono kutoka kwa viongozi wa EU.

    Pia anaelezea jibu la Israeli kwa shambulio la Hamas la Oktoba kama "kutokuwa na uwiano kabisa". Sánchez amekuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Israel tangu ilipoanzisha mashambulizi yake ya kijeshi kujibu mashambulizi ya Hamas ya tarehe 7 Oktoba.

    Matamshi yake ya hivi karibuni ni baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia Penny Wong, ambaye amependekeza nchi hiyo inaweza kutambua utaifa wa Palestina ili kuongeza kasi ya kuelekea amani.

  6. Watu wawili wauawa katika shambulizi linaloshukiwa kuwa la al-Shabaab nchini Kenya

    h

    Chanzo cha picha, Taifa Leo

    Watu wawili wameripotiwa kuuawa na magari mawili kuteketezwa baada ya kushambuliwa na watu wanaoshukiwa kuwa ni wanamgambo wa al-Shabaab katika mji wa pwani wa Lamu nchini Kenya.

    Al-Shabab imekuwa ikifanya mashambulizi katika maeneo ya Pwani na Kaskazini-Mashariki mwa Kenya yanayopakana na Somalia wakati wa mwezi wa Ramadhani.

    Somalia imeomba msaada zaidi kutoka kwa Umoja wa Afrika ili kupambana na kundi hilo lenye uhusiano na al-Qaeda.

  7. Tazama: Ndege 14 kutoka mataifa tisa zikidondosha tani 10 za misaada Gaza

    Maelezo ya video, Tazama: Ndege 14 kutoka mataifa tisa zikidondosha tani 10 za misaada Gaza

    Ndege kubwa zaidi ya kijeshi ya muungano wa kijeshi tangu kuanza kwa vita hivyo imekabidhiwa Gaza.

    Ndege 14 kutoka mataifa tisa yakiwemo Uingereza, Marekani, Uholanzi, Ujerumani, Misri, Indonesia, UAE na Ufaransa, ziliangusha tani 10 za msaada ambazo ni pamoja na chakula na maji.

    Kiwango cha utoaji wa huduma hiyo kilipangwa kuashiria mwisho wa mwezi wa Ramadhani na shughuli hiyo ilizinduliwa katika kambi ya kijeshi mjini Amman, mji mkuu wa Jordan.

  8. Israel Gaza: Netanyahu anafanya 'kosa', asema Biden

    h

    Chanzo cha picha, Reuters

    Rais wa Marekani Joe Biden amesema anaamini kuwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anafanya "kosa" katika kulishughulikia suala la mzozo wa Gaza.

    "Nadhani anachofanya ni makosa. Sikubaliani na mbinu yake," alisema kwenye mahojiano.

    Alisema Gaza inapaswa kuwa na " kupata kikamilifu chakula na dawa zote" kwa muda wa wiki sita hadi nane zijazo.

    Wiki iliyopita alitahadharisha kwamba uungwaji mkono unaoendelea wa Marekani wa vita hivyo unategemea Israel kuruhusu chakula na dawa zaidi.

    Israel imekanusha kuzuia kuingia kwa msaada au usambazaji wake ndani ya Gaza, na imeshutumu mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kuwa msingi wa kushindwa kupata misaada ambayo inaruhusiwa kwa watu wanaohitaji.

    Mazungumzo ya wiki kadhaa yameshindwa kuleta makubaliano ya kusitisha mapigano lakini shinikizo la kimataifa linaongezeka.

    Mahojiano hayo ya saa moja yalirekodiwa Jumatano iliyopita - siku chache baada ya mashambulizi ya kijeshi ya Israel kuwaua wafanyakazi saba wa kutoa misaada na World Central Kitchen - na yalipeperushwa Jumanne usiku kwenye mtandao wa Marekani unaotumia lugha ya Kihispania, Univision.

    Bw Biden alisema ni jambo la kukasirisha jinsi magari ya shirika la misaada yalivyokuwa "yamepigwa na ndege zisizo na rubani na kutolewa kwenye barabara kuu".

    Vikosi vya Ulinzi vya Israeli tangu wakati huo vimesema "makosa makubwa" yalisababisha kulengwa kwa wafanyakazi. Uchunguzi kuhusu mashambulio hayo ulipelekea maafisa wawili wakuu kufutwa kazi.

    Katika mahojiano hayo Bw Biden alisema: "Ninatoa wito kwa Waisraeli kutoa wito tu wa kusitishwa kwa mapigano, ili kuruhusu kwa muda wa wiki sita, nane zijazo, upatikanaji kamili wa chakula na dawa zote zinazoingia nchini."

  9. Shughuli ya utafutaji yaendelea baada ya mlipuko mbaya kwenye kiwanda cha kuzalisha umeme Italia

    h

    Chanzo cha picha, Vigili del Fuoco

    Maelezo ya picha, Picha kutoka Vigili Del Fuoco zinaonyesha muonekano kutoka angani wa mtambo wa kuzalisha umeme huku moshi ukiongezeka

    Watu wanne wamefariki na wengine kadhaa hawajulikani walipo kufuatia mlipuko uliotokea kwenye kinu cha kuzalisha umeme kwa maji kaskazini mwa Italia.

    Mlipuko huo ulitokea chini ya maji kwenye kiwanda katika Ziwa Suviana, kilomita 70 kutoka mji wa Bologna.

    Eneo lililoathiriwa liko 30m (100ft) chini ya uso wa ziwa.

    Watu wanne wamefariki na wengine kadhaa hawajulikani walipo kufuatia mlipuko uliotokea kwenye kinu cha kuzalisha umeme kwa maji kaskazini mwa Italia.

    Mlipuko huo ulitokea chini ya maji kwenye kiwanda katika Ziwa Suviana, kilomita 70 kutoka mji wa Bologna.

    Eneo lililoathiriwa liko 30m (100ft) chini ya uso wa ziwa.

  10. Wazazi wa kijana aliyewapiga risasi wenzake shuleni wahukumiwa kifungo kisichopungua miaka 10

    j

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Hukumu ya miaka saba ilipendekezwa, lakini waendesha mashtaka waliomba iongezwe.

    James na Jennifer Crumbley, wazazi wa kijana huyo walionekana pamoja kwa mara ya kwanza baada ya miezi kadhaa wakati wa kusikilizwa kwa hukumu ya kesi hiyo, Jumanne.

    Wote wawili walionyesha majuto juu ya shambulizi lililotekelezwa na mtoto wao, huku mawakili wao wakishinikiza kupunguza kifungo chao gerezani.

    Katika kesi hiyo ya kihistoria, majaji tofauti walimpata kila mzazi wa kijana huyo, Ethan Crumbley na hatia ya kuua bila kukusudia mapema mwaka huu.

    Jaji Cheryl Matthews alisema kuwa hukumu iliyoongezwa ya miaka 10 hadi 15 ilikuwa "kama onyo" na ilionyesha kushindwa kwa wazazi kusitisha shambulio hilo.

    Wazazi hao wanaweza kupata msamaha baada ya kutumikia kifungo cha miaka 10 gerezani, lakini hawawezi kuzuiliwa kwa zaidi ya miaka 15 ikiwa msamaha utakataliwa.

    Waendesha mashtaka walidai wawili hao walikuwa wamepuuza dalili za wazi kwamba afya ya akili ya mtoto wao ilikuwa imezorota, na wakabainisha kwamba walimnunulia Ethan Crumbley bunduki aliyotumia katika shambulio la 2021.

    Mtoto wao wa kiume alikuwa na umri wa miaka 15 alipowaua wanafunzi wanne kwa bunduki katika Shule ya Upili ya Oxford. Wengine saba walijeruhiwa kwa risasi.

  11. Israel Gaza: Australia yaashiria kuwa inaweza kulitambua taifa la Palestina

    h

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Maoni ya Penny Wong yanafuatia matamshi sawa na yale yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Cameron

    Waziri wa mambo ya nje wa Australia aamedokeza kuwa nchi hiyo inaweza kutambua uraia wa Palestina, ili kuongeza kasi ya kuelekea amani.

    Hata hivyo Hamas haiwezi kuwa na nafasi katika utawala wake, Penny Wong alisema.

    Upinzani wa Australia na Shirikisho la Wazayuni la Australia wanasema hatua kama hiyo itakuwa imechukuliwa mapema.

    Canberra imesema kwa muda mrefu kwamba kutambuliwa kwa taifa la Palestina kunaweza tu kuja kama sehemu ya suluhisho la mataifa mawili lililofikiwa na Israeli.

    Lakini maoni ya Bi Wong yanalingana na hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Cameron mapema mwaka huu, ambapo alidokeza kwamba Uingerereza pia inaweza kutambua taifa la Palestina bila kuungwa mkono na Israel.

    Serikali ya Australia katika miezi ya hivi karibuni imezidi kuelezea wasiwasi wake juu ya vita dhidi ya Hamas huko Gaza - ikiwa ni pamoja na baada ya mfanyakazi wa misaada wa australia kuuawa pamoja na wengine sita wakati wa mashambulizi ya anga ya Israel.

    Katika hotuba yake Jumanne usiku, Bi Wong alisema suluhisho la mataifa mawili - ambapo Waisraeli na Wapalestina waliishi bega kwa bega katika nchi tofauti - ndio "tumaini pekee la kuvunja mzunguko usio na mwisho wa ghasia".

  12. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara leo ikiwa ni tarehe 10.05.2024