Meli ya kwanza iliobeba chakula yawasili ufukweni Gaza
Meli ya kwanza iliyokuwa ikivuta mashua ya misaada ya kibinadamu hadi Gaza imepakua vifaa ufukweni.
Moja kwa moja
Mwanamke afariki baada ya kukimbizwa na dubu

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwanamke mwenye umri wa miaka 31 amefariki baada ya kukimbizwa na dubu kaskazini mwa Slovakia, maafisa wamesema.
Taasisi ya Huduma ya Uokoaji katika Milima ya Slovakia imesema mwili wa mwanamke huyo uliokotwa kutoka msituni katika milima ya Low Tatras nchini Slovakia Ijumaa jioni.
Mwanamke huyo alikuwa akitembea na mwenzake wa kiume wakati walipokutana na dubu.
Kwa mujibu wa mwanaume aliyekuwa naye amesema walikimbia kuelekea njia tofauti.
Eneo hilo lina misitu mingi na miteremko mikali.
Mamlaka ya Kislovakia ilisema kuwa wawili hao walikuwa wakitembea katika Bonde la Demänovská walipofukuzwa na Dubu.
Mwili wa mwanamke huyo uligunduliwa na mbwa wa upekuzi muda mfupi baada ya mwenziake wake kwenda kuomba msaada.
Dubu huyo alikuwa bado karibu, na alitishwa kwa milio yarisasi iliyopigwa na Huduma ya Uokoaji Milimani.
'Madaktari wanatushauri kutafuta kazi nje ya nchi'
Maelezo ya video, 'Madaktari wanatushauri kutafuta kazi nje ya nchi’ Madaktari nchini Kenya wamegoma kwa muda usiojulikana kwasababu serikali imeshindwa kuwaajiri Madaktari watarajali pamoja na uwepo wa mazingira duni ya kazi.
Shirley na Micheni ni miongoni mwa Madaktari tarajali zaidi ya 1,000 wanaosubiri kupangiwa kazi. Huku , Serikali inasema haina pesa za kuwaajiri.
Taarifa hii imetayarishwa na Carolyne Kiambo na Dorcas Wangira Picha:Jeff Sauke
Wakenya wanaweza kurejea kulipa ushuru wa nyumba mwezi huu iwapo Ruto atasaini mswada Jumatatu

Chanzo cha picha, EPA
Serikali inaweza kuanza tena kukata asilimia 1.5 ya ushuru wa Nyumba Nafuu kuanzia mwisho wa mwezi huu.
Haya yanajiri huku Rais William Ruto akisema kuwa Jumatatu atatia saini kuwa sheria Mswada wa Nyumba za Gharama Nafuu uliorekebishwa, 2023, unaozingatia sababu ambazo mahakama ilitaja ilipotangaza kuwa ni kinyume na katiba.
Ruto alikuwa akizungumza katika eneo bunge la Chepalungu, Kaunti ya Bomet, ambapo aliandamana na viongozi kadhaa akiwemo naibu wake Rigathi Gachagua, Waziri wa Barabara Kipchumba Murkomen na Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah.
“Jumatatu naenda kuweka sahihi sheria mpya ya Affordable Housing ndio tuhakikishe ya kwamba tumeweka msingi dhabiti...tuhakikishe ya kwamba by next year tuwe na vijana elfu mia tatu ambao watakuwa wanafanya kazi kwa program ya Affordable Housing,” alisema.
Mahakama Kuu mnamo Novemba 28, 2023 ilitangaza ushuru wa nyumba kuwa kinyume na katiba, na kuamua kuwa ulikiuka Kifungu cha 10, 2 (a) cha Katiba.
Ndege aina ya Boeing yatua salama bila sehemu ya bawa

Chanzo cha picha, Getty Images
Sehemu ya bawa iliyotoka kwenye ndege ya Boeing iligunduliwa baada ya ndege kutua kwenye uwanja wa ndege katika jimbo la Oregon nchini Marekani siku ya Ijumaa, ilisema United Airlines.
Msemaji amesema ndege ya United 433 iliondoka San Francisco na kufika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rogue Valley huko Medford, Oregon, karibu 11:30 (18:30 GMT) siku ya Ijumaa. Ndege hiyo aina ya Boeing 737-800 ambayo inatumika kwa miaka 25 sasa ilikuwa imebeba abiria 139 na wafanyakazi 6.
Hakuna aliyejeruhiwa ingawa sehemu hiyo iliyopotea halikutambuliwa wakati wa safari ya ndege.
Boeing iko chini ya uangalizi mkali baada ya mfululizo wa matukio ya kiusalama.
Amber Judd, afisa mkuu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rogue Valley Medford, alisema ndege hiyo ilitua salama na sehemu hiyo ya ndege kupotea iligunduliwa tu wakati wa ukaguzi wa baada ya safari ya ndege.
"Tutafanya uchunguzi wa kina katika ndege hii na kufanya matengenezo yote yanayohitajika kabla ya kurejea kufanya kazi," alisema. Uchunguzi utafanywa "ili kuelewa vyema jinsi uharibifu huu ulivyotokea", aliongeza. Sehemu ya bawa iliyokosekana ilikuwa karibu na vifaa vya kutua, chini ya ndege, kulingana na picha za ndege kwenye mitandao ya kijamii.
Ndege zote zinazotoka na zinazoingia zilisitishwa kwa muda kwenye uwanja wa ndege kutafuta sehemu hiyo ya ndege.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Marekani (FAA) ilisema inachunguza jinsi sehemu hiyo lilivyotengana.
Soma zaidi:
- Ndege ya Boeing 737 ya Sriwijaya Air Indonesia, Jakarta imepoteza mawasiliano baada ya kupaa
Fahamu jinsi dini nyingine zinavyotekeleza ibada ya kufunga
Maelezo ya video, Fahamu jinsi dini nyingine zinazotekeleza ibada ya kufunga Ibada ya kufunga ama saumu inayoendelea katika mwezi huu Ramadhan inatekelezwa na waumini wa dini ya Kiislamu.
Hata hivyo dini nyingine pia kama Orthodox,wakristo na wahindu pia wao wana ibada tofauti ya kufunga.
Jaji Mkuu wa Kenya ashinda tuzo ya kiongozi bora wa kike wa Mwaka barani Afrika 2023

Chanzo cha picha, JUDICIAL SERVICE
Jaji Mkuu wa Kenya Martha Koome ametunukiwa tuzo ya Kiongozi Bora wa Kike wa Mwaka wa Afrika 2023 wakati wa hafla iliyofanyika Addis Ababa, Ethiopia.
Katika hotuba yake ya kukubali tuzo hiyo, bi Koome alisema kuwa utambuzi huo uliashiria kujitolea kwa pamoja na uthabiti wa watu binafsi wanaojitahidi kupata ubora katika bara zima.
"Tuzo hii sio yangu peke yangu. Ni sifa ninayojitolea kwa moyo wote kwa taasisi niliyobahatika kuongoza, Idara ya Mahakama ya Kenya,” Koome alisema.
"Kutambuliwa huku kunatuchochea kuendelea kutafuta uongozi bora na kuongeza bila kuchoka ubora wa utoaji wa huduma kwa taasisi zetu," Koome alisema.
Wakati huo huo Rais Mstaafu wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alitunukiwa tuzo ya kiongozi bora kwa mwaka 2023 katika upande wa amani na usalama wa bara la Afrika.
Msaada wa chakula kutoka Marekani wazua gumzo mitandaoni Tanzania

Chanzo cha picha, USA
Maelezo ya picha, Msaada wa chakula kutoka Marekani Mzozo umeibuka katika mitandao ya kijami nchini Tanzania baada ya serikali ya Marekani kwa ushirikiano na jumuiya za kimataifa kutoa msaada wa chakula kwa shule zilizopo mjini Dodoma.
Msaada huo unashirikisha mchele ulioongezwa virutubisho, maharage na mafuta ya alizeti kutoka kwa wakulima wa Marekani
Kulingana na Marekani mpango huo unaakisi ahadi na dhamira ya dhati ya Marekani ya kukuza afya, elimu, na fursa kwa watoto kote ulimwenguni.
Hatahivyo hatua hiyo haikupokelewa vyema na watumiaji wa mitandao nchi humo waliohoji iwapo taifa hilo linahitaji msaada wa chakula
Elias G balimponyakatika mtandao wake wa X alihoji: Hivi Tanzania tunahitaji msaa wa chakula kweli? Aliongezea: Chakula??? MAHARAGWE, MCHELE, MAFUTA YA ALIZETI??
Alisema: Ndugu zangu Marekani njooni tushirikiane katika mambo mengine muhimu ya kuinua uchumi. Tanzania kusaidiwa chakula HAPANA . Natamani kumfahamu kiongozi wangu aliyeomba msaada wa CHAKULA. Jamaa huyo badala yake aliitaka Marekani kutoa misaada kama hiyo kwa taifa la Sudan
Kwa upande mwengine mtumiaji mwengine wa mtandao wa X kwa jina CAT POWER alishutumu hatua hiyo akitaka waziri aliyepokea msaada huo kufutwa kazi mara moja..
Alisema kwamba Tanzania ni mlimaji mkubwa wa mchelele wa kutosha hadi unakosa soko. Alihoji ni vipi watumie mchele wenye virutubishi kutoka Marekani?.
Mtumiaji mwengine wa mtandao wa X kwa jina Lings, aliuliza maswali kadhaa. Je tumefika huku? Ni kweli tuliomba hiki chakula? Je tunakufa njaa? Hatuwezi kulisha watoto wetu? Mchele? Kweli Mchele? Kwanini wasipeleke nchi zenye njaa?
Aliendelea kusema: Nina hakika kwamba hatukuomba wala hatuhitaji, Wanatupa michele?
Mwengine kwa jina Yoab Mwana wa Seruya alisema: Tunashukuru lakini, HAPANA hatuhitaji huu mchele. Alisema Mchele wetu wa Mbeya upo wa kutosha sana. Alitaka msaada huo wa chakula kupelekwa katika kambi za wakimbizii huko Kigoma .
Aliongezea: Au pelekeni Sudan Kusini .Sisi Hatuutaki. Taifa letu linajitosheleza kwa Chakula alihitimisha.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Meli ya kwanza iliobeba msaada wa chakula yawasili ufukweni Gaza

Chanzo cha picha, Reuters
Meli ya kwanza iliyokuwa ikivuta mashua ya misaada ya kibinadamu hadi Gaza imepakua vifaa ufukweni.
Meli ya Open Arms ya Uhispania iliondoka Cyprus siku ya Jumanne ikiwa na tani 200 za chakula zikihitajika sana kwa Gaza, ambayo Umoja wa Mataifa unasema inakabiliwa na njaa
Video zilizochapishwa mtandaoni zinaonyesha korongo ikisogeza kreti kutoka kwenye jahazi hadi lori zikingoja kwenye gati iliyojengwa kimakusudi.
Inaashiria kuanza kwa jaribio la kuona kama usafirishaji baharini unafaa, baada ya usafirishaji wa ndege na nchi kavu kuwa mgumu.
Jiko Kuu la Dunia (WCK), ambalo lilisambaza chakula hicho, lilifanya kazi hiyo kwa ushirikiano na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kupeleka shehena ya majahazi ya mchele, unga, kunde, mboga za makopo na protini za makopo.
Natumai hujambo


