Tukio jingine la uvujaji wa gesi lahofiwa siku chache baada ya mlipuko mbaya nchini Kenya
Mnamo Jumatatu, shule katika mtaa wa Embakasi pia zimewataka wazazi kuwachukua watoto wao.
Moja kwa moja
Abdalla Seif Dzungu, Dinah Gahamanyi and Yusuf Jumah
Celine Dion ajitokeza kwa kushtukiza kwenye tuzo za Grammy

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Celine Dion alishangiliwa wakati akipanda jukwaani kwenye tuzo za Grammy Celine Dion alijitokeza bila kutarajiwa kwenye tuzo za Grammy huku akikabilianana ugonjwa wa nadra wam fumo wa neva unaofahamika kama Stiff Person Syndrome.
Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 55 alishangiliwa pakubwa kubwa alipopanda jukwaani kutoa tuzo ya albamu bora ya mwaka.
"Asanteni nyote... Ninaposema kwamba nina furaha kuwa hapa, ninamaanisha kutoka moyoni mwangu," Dion alisema.
Alitoa tuzo kwa Taylor Swift kwa albamu yake Midnights.
Mwimbaji huyo wa wimbo My Heart Will Go On aliandamana jukwaani na mwanaye kuwasilisha tuzo kubwa zaidi ya usiku wa mwaka, miaka 27 baada ya Diana Ross na Stinger kumpa tuzo hiyo, alisema.
"Wale ambao wamebarikiwa vya kutosha kuwa hapa kwenye tuzo za Grammy hawapaswi kamwe kuichukulia kuwa jambo la kawaida, ni upendo na furaha kubwa ambayo muziki huleta katika maisha yetu na kwa watu kote ulimwenguni," alisema.
Soma zaidi:
- Ifahamu hali ya kukaza misuli inayomkumba Celine Dion
Lysychansk: Makumi ya watu wameuawa katika shambulizi dhidi ya mji wa Ukraine unaoshikiliwa na Urusi

Chanzo cha picha, SSIAN EMERGENCIES MINISTRY
Urusi imesema takriban watu 28 wwameuawa katika shambulio lililotokea kwenye duka la mikate katika mji wa Lysychansk mashariki mwa Ukraine unaokaliwa na Urusi.
Jengo hilo, ambalo pia lilikuwa na mgahawa unaoitwa Adriatic, lilipigwa Jumamosi.
Maafisa wa Urusi wamesema wanajeshi, wanawake na mtoto waliuawa katika shambulio hilo.
Utawala wa Urusi umesema silaha zilizotolewa na nchi za Magharibi zilitumika katika shambulio hilo, ambalo imeliita "kitendo cha kigaidi" cha Ukraine.
Kyiv haijatoa maoni yake, lakini wanablogu wa kijeshi wa Ukraine wamedai tangu wakati huo "washirika" na maafisa wa Urusi walikuwa kwenye jengo hilo wakati huo.
Siku ya Jumatatu, mkuu wa Jamhuri ya Watu wa Luhansk (LNR) iliyounganishwa na Urusi alisema kuwa shambulizi hilo lilimuua waziri wa hali ya dharura, Alexey Poteleshchenko, ambaye alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwenye mgahawa uliopigwa.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Maria Zakharova alisema kuwa Jeshi la Ukrain lililenga duka la mikate kwa makusudi, wakijua kwamba "wenyeji kwa kawaida huja huko Jumamosi kununua mikate na mboga, ikiwa ni pamoja na wazee na familia zilizo na watoto".
Hakuna idadi ya vifo au madai yoyote ya Urusi au Ukraine ambayo yamethibitishwa na BBC.
Pakistan: Takriban watu 10 wameuawa katika shambulizi katika kituo cha polisi

Chanzo cha picha, EPA
Takriban maafisa 10 wameuawa katika shambulio la saa moja kwenye kituo cha polisi nchini Pakistan.
Maafisa hao walipoteza maisha baada ya zaidi ya wanamgambo 30 kufanya shambulizi hilo mapema Jumatatu.
Wengine wanne walijeruhiwa katika mapigano hayo yaliyodumu kwa saa mbili na nusu, mkuu wa polisi wa jimbo la Khyber Pakhtunkhwa aliambia shirika la habari la AFP.
Haijabainika ni nani alihusika na shambulio hilo, au ikiwa inahusiana na uchaguzi uliofanyika Alhamisi.
Kumekuwa na ongezeko la ghasia katika wiki chache zilizopita, ikiwa ni pamoja na mgombea ubunge wa Kitaifa kuuawa kwa kupigwa risasi katika sehemu nyingine ya Khyber Pakhtunkhwa Jumatano iliyopita.
Hata hivyo, Khyber Pakhtunkhwa pia ina historia ndefu ya mashambulizi dhidi ya shabaha za serikali na usalama, pamoja na raia, na kundi la Taliban la Pakistan, Islamic State na makundi mengine ya wanamgambo.
Kulingana na Akhtar Hayat Gandapur, mkuu wa polisi wa eneo hilo, mashambulizi hayo yalianzishwa mwendo wa saa 03:00 kwa saa za huko Jumatatu (22:00 GMT Jumapili), kwanza kwa milio ya risasi, ikifuatiwa na maguruneti.
Wanamgambo hao walishambulia kutoka pande tatu tofauti, na kwa muda mfupi walikuwa na udhibiti wa kituo cha polisi, aliongeza.
Shambulio la ndege zisizo na rubani laua wapiganaji sita wanaoongozwa na Wakurdi katika kambi ya Marekani nchini Syria

Chanzo cha picha, Reuters
Kwa wakati huu wa mvutano uliokithiri kote Mashariki ya Kati, tunajaribu kukuletea habari kutoka maeneo kadhaa - na haya mapya zaidi yanatoka Syria.
Shambulizi la ndege zisizo na rubani katika kambi kubwa zaidi ya kijeshi ya Marekani limewaua takriban wapiganaji sita kutoka kwa wanamgambo washirika wanaoongozwa na Wakurdi.
Jeshi la Kidemokrasia la Syria (SDF) chombo cha ngani kisichokuwa na rubani (UAV) kilichorushwa kutoka eneo linalodhibitiwa na serikali ya Syria liligonga chuo chake cha makomando katika eneo la mafuta la al-Omar katika mkoa wa mashariki.
Kundi la SDF - ambalo lilisaidia muungano unaoongozwa na Marekani kushinda kundi la Islamic State mashariki mwa Syria - liliongeza kuwa uchunguzi wa awali uligundua kuwa wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran ndio waliohusika na "kitendo cha kigaidi".
Shirika la Uangalizi wa Haki za Kibinadamu la Syria (SOHR) lenye makao yake makuu nchini Uingereza, limeripoti kuwa makomando saba wa SDF waliuawa na 18 kujeruhiwa katika shambulio lililotajwa kuwa ni la 108 la wanamgambo kwenye kambi za Marekani nchini humo tangu katikati ya Oktoba.
Kundi la Islamic Resistance in Iraq - kundi chini ya mwavuli wa wanamgambo wa Iraq wanaoungwa mkono na Iran - lilidai shambulio la ndege isiyo na rubani siku ya Jumapili "dhidi ya kituo kinachokaliwa na Marekani katika eneo la mafuta la al-Omar" katika taarifa iliyoripotiwa na vyombo vya habari vya Iraq.
Pia ilidai shambulizi la ndege zisizo na rubani kwenye kambi ya 22 ya Marekani upande wa Jordan kwenye mpaka wa Syria tarehe 28 Januari, ambalo liliua wanajeshi watatu wa Marekani na kusababisha Marekani kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya vituo vya jeshi la Iran na wanamgambo wanaoungwa mkono Iran nchini na Syria na Iraq.
Mwanamke afariki wakati akijaribu kuwatuliza watoto wa mbwa – binti

Chanzo cha picha, Family Handout
Maelezo ya picha, Familia ya Esther Martin ilisema alikuwa muathirika wa shambulio la mbwa wa XL katika kijiji kilichopo kando ya bahari Mwanamke mmoja amefariki baada ya kushambuliwa na mbwa alipokuwaakijaribu kuwatuliza watoto wa mbwa waliokuwa wasumbufu kwa kutumia ufagio, binti yake anasema.
Esther Martin, 68, alifariki katika eneo la Jaywick, karibu na Clacton-on-Sea, Essex, nchini Uingereza Jumamosi alipokuwa amekwenda kumtembelea mjukuu wake.
Mwanamume mwenye umri wa miaka 39 ameachiliwa kwa dhamana kwa tuhuma za makosa hatari ya mbwa na wanyama hao wawili wauliwa.
Binti yake Bi Martin ameiambia BBC kuwa wanyama hao walikuwa ni aina ya mbwa wa XL waliopigwa marufuku, lakini polisi wanasema wanasubiri mifugo hao wathibitishwe wataalamu.
"Kulikuwa na mbwa wakorofi wa XL katika eneo hilo, na mama yangu alikuwa ameelezea wasi wasi wake kuhusu mbwa hao kuwa ni hatari na wakali," alisema.
"Pia kulikuwa na vitoto sita vya mbwa."
Bi Martin anasema vitoto hivyo vilikuwa vikipigana, na kwamba mama yake aliambiwa na mwenye mbwa mapema "kuwa kutumia ufagio akiwafukuza kulikuwa ni kuwavuruga". "Hapo ndipo aliposhambuliwa," alisema.
Goma - DRC: 'Kuna hofu na wasiwasi mwingi' wanahofia kuwa M23 wanaweza 'kuuteka' mji

Chanzo cha picha, GOUVERNORAT NORD KIVU
Baadhi ya wakazi wa Goma, mji mkuu wa Mkoa wa Kivu Kaskazini, wanasema wanahofia kwamba waasi wa M23 sasa wanalenga kuuzingira mji huo na kuufanya usiweze kufukiwa.
Hii ni baada ya M23 kusema kuwa inadhibiti kituo cha Shasha kwenye barabara kuu ya Goma-Sake-Minova-Bukavu.
Kwa kawaida, Goma – mji uliopo kando ya Ziwa Kivu, hupata zaidi ya 90% ya chake hutoka maeneo ya jirani ya Rutshuru na Masisi, ambayo yanayopatakana na barabara kuu nne zifuatazo:
- Goma – Rutshuru – Butembo (pia kwenda/kutoka mpaka wa Bunagana)
- Goma – Sake – Masisi Kati (Masisi Centre)
- Goma – Sake – Kitchanga
Kundi la M23 linasema linadhibiti maeneo ya karibu na Sake, na Norbert Nangaa, mkuu wa kundi la AFC na M23, alionekana kwenye video akisema kuwa siku ya Ijumaa "majeshi yangu yaliiteka Shasha, na kuizingira Sake".
Barabara tatu za kwanza sasa zinapita katika maeneo yanayodhibitiwa na M23, na kwa sasa sasa sio njia zinazofaa kutumiwa na raia kwenda au kutoka Goma.

Chanzo cha picha, Google
Maelezo ya picha, Barabara nne, zikiwemo tatu zinazokutana Sake, ndizo vyanzo vikuu vya mapato kwa wakazi wa Goma Juhudi za BBC za kuzungumza na vikosi vya serikali hazikufua dafu, na hadi sasa hakuna taarifa rasmi kutoka upande huo kuhusu mapigano makali ambayo yamedumu kwa siku kadhaa na kuendelea mwishoni mwa juma.
Baadhi ya vyombo vya habari vilitangaza Jumatatu kuwa vikosi vya serikali vitarejea katikati ya Shasha, jambo ambalo bado halijathibitishwa na upande wa serikali.
Wakaazi watoroka eneo la mlipuko wa gesi Nairobi kutokana na madai ya uvujaji wa gesi

Chanzo cha picha, Online
Siku tatu baada ya mlipuko kutokea eneo la Embakasi, wakaazi wameanza kutoroka eneo hilo tena kwa tuhuma za uvujaji wa gesi safi.
Ripoti za uvujaji wa gesi hiyo mpya zilianza kusambazwa Jumatatu, Februari 5, asubuhi na kuwalazimu watu kutafuta usalama katika maeneo jirani.
Serikali ya Kaunti ya Nairobi imewahakikishia wakaazi wa Embakasi kuwa eneo hilo ni salama kwani tayari wataalamu walikuwa wamedhibiti hali hiyo.
"Ni tahadhari tumechukua kwani tumeiita Mamlaka ya Kudhibiti Kawi na Petroli (EPRA) ili kubaini iwapo kuna tishio," Bramwel Simiyu, Afisa Mkuu wa Usimamizi wa Majanga wa Nairobi alinukuliwa akisema.
"Kuna ripoti kwamba kulikuwa na moto. Tumeweka huduma zetu katika hali ya dharura lakini hadi sasa hakuna sababu ya kutisha."
Bramwel Simiyu alihakikishia umma kuwa hakuna moto mpya uliotambuliwa na kwamba Serikali ya Kaunti itahakikisha kuwa kuna usalama kwa Wakenya.
Kwa picha: Houthi wafanya maandamano mjini Sanaa

Chanzo cha picha, Reuters
Mwishoni mwa juma, Waasi wa Houthi wa Yemen walifanya maandamano nje kidogo ya mji mkuu Sanaa kupinga mashambulizi mapya ya Marekani dhidi yao, na kwa mshikamano na Wapalestina.
Wahouthi wamejulikana kwa maandamano makubwa, ambayo mara nyingi hushuhudia kujitokeza kwa mamia ya maelfu ya watu.
Edmund Fitton-Brown, ambaye alikuwa balozi wa Uingereza nchini Yemen kuanzia 2015-17, hivi majuzi aliambia BBC kwamba Wahouthi huleta makundi ya watu mitaani kwa hofu.

Chanzo cha picha, getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images
Mlipuko wa gesi Nairobi: Idadi ya waliofariki yafikia 6

Watu watatu zaidi wamefariki dunia kutokana na majeraha waliyoyapata wakati wa mlipuko wa gesi ya Embakasi, na kufanya idadi ya watu waliofariki dunia kufikia sita kufikia sasa kutokana na tukio hilo.
Taarifa ya Msemaji wa Serikali Isaac Mwaura inaeleza kuwa watu wengine saba wako katika hali mahututi katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) na Hospitali ya Kufundisha, Rufaa na Utafiti ya Chuo Kikuu cha Kenyatta (KUTRRH).
KUTRRH imeshuhudia jumla ya wagonjwa 27, huku wanane wakiwa tayari wameruhusiwa na 19 wapo chini ya uangalizi, wakiwemo wanaume 10, wanawake sita na watoto wadogo watatu.
Miongoni mwao, mgonjwa mmoja yuko katika hali mbaya kutokana na kuungua sana na majeraha ya kuvuta pumzi. Mama mjamzito na mtoto mdogo wa miaka 4 pia wanapokea matibabu.
Hospitali ya KNH ilipokea wagonjwa 67 wa tukio hilo, huku sita wakiwa katika hali mbaya.
Je ni kipi kinachoendelea Mashariki ya kati?

Chanzo cha picha, Reuters
- Usiku kucha, jeshi la Marekani lilifanya mashambulizi zaidi dhidi ya kundi la Houthi nchini Yemen
- Afisi ya (Centcom) Marekani ilisema katika taarifa yake kwamba vikosi vyake vilishambulia kombora la ardhini na makombora manne ya kuzuia meli ambayo "yalitayarishwa kurushwa dhidi ya meli katika Bahari ya Shamu"
- Ilikuwa ni awamu ya pili ya mashambulizi nchini Yemen mwishoni mwa juma - baada ya Marekani kufanya kazi na jeshi la Uingereza kutekeleza mashambulizi kama hayo ya anga siku ya Jumamosi.
- Mashambulizi ya Jumamosi ya pamoja ya Marekani na Uingereza yalipamba angani usiku kusini mwa mji mkuu wa Yemen wa Sana'a, huku mwanaharakati mmoja wa haki za binadamu na mkazi wa eneo hilo akiambia BBC kuwa nyumba zinatetemeka.
- Mashambulizi hayo yanafuatia kuendelea kwa mashambulizi ya kundi linaloungwa mkono na Iran katika Bahari ya Shamu dhidi ya meli za kijeshi na kibiashara
- Mashambulizi ya Houthis yamelazimisha makampuni makubwa ya meli kuepuka njia muhimu za maji, na kuathiri biashara ya kimataifa kwa kulazimisha meli kuchukua safari ndefu kuzunguka Pembe ya Afrika hadi Ulaya.
- Maafisa wa Houthi walikaidi mashambulizi yaliyoongozwa na Marekani - na kuapa kujibu.
- Akijibu mashambulio ya Jumamosi, msemaji wa jeshi la kundi hilo, Yahya Sarea, aliandika kwenye X: "Mashambulizi haya hayatatuzuia kutoka kwa msimamo wetu wa kiadili, kidini na wa kibinadamu wa kuunga mkono watu wa Palestina walio na uthabiti katika Ukanda wa Gaza na hayatapita bila jibu au bila kuadhibiwa.
Yang Hengjun: Mwandishi wa Australia apewa hukumu ya kifo iliyositishwa nchini Uchina

Chanzo cha picha, YANG HENGJUN/TWITTER
Mwandishi wa Australia Yang Hengjun amepewa hukumu ya kifo iliyosimamishwa kwa muda na mahakama ya Uchina, miaka mitano baada ya kukamatwa na kushtakiwa kwa ujasusi.
Hukumu hiyo inaweza kubadilishwa na kuwa kifungo cha maisha baada ya miaka miwili, kulingana na maafisa wa Australia.
Dk Yang - msomi na mwandishi wa riwaya ambaye aliandika blogi kuhusu masuala ya serikali ya Uchina - anakanusha mashtaka, ambayo hayajawekwa wazi.
Serikali ya Australia inasema "imeshtushwa" na matokeo hayo.
Waziri wa Mambo ya Nje Penny Wong amemwita Balozi wa China nchini Australia kwa maelezo, na Jumatatu alisema serikali "itawasiliana" na jibu lake kwa Beijing "kwa maneno makali".
"Tumetoa wito mara kwa mara wa viwango vya msingi vya haki, usawa wa kiutaratibu na kutendewa kwa ubinadamu kwa Dk Yang, kwa mujibu wa kanuni za kimataifa na wajibu wa kisheria wa China," alisema katika taarifa yake.
"Waaustralia wote wanataka kuona Dkt Yang akiunganishwa tena na familia yake. Hatutalegea katika utetezi wetu."
Maafisa wa Australia hapo awali walitoa wasiwasi kuhusu matibabu yake, lakini wizara ya mambo ya nje ya China imewaonya kutoingilia kesi hiyo, na kuheshimu "uhuru wa mahakama" ya taifa hilo.
Wafuasi wa Dk Yang wameelezea kuzuiliwa kwake kama "mateso ya kisiasa".
"Anaadhibiwa na serikali ya Uchina kwa ukosoaji wake wa ukiukaji wa haki za binadamu nchini Uchina na utetezi wake wa maadili ya ulimwengu kama vile haki za binadamu, demokrasia na sheria," rafiki yake, msomi wa Sydney Feng Chongyi, aliiambia BBC.
Dk Yang, ambaye hapo awali alifanya kazi katika Wizara ya Usalama ya Nchi ya China, alipewa jina la utani "mchuuzi wa demokrasia" lakini maandishi yake mara nyingi yaliepuka ukosoaji wa moja kwa moja wa serikali.
Alikuwa akiishi New York lakini alisafiri hadi Guangzhou mnamo Januari 2019 na mkewe na mtoto wake - wote raia wa Uchina - kwa kupewa visa wakati alipokamatwa kwenye uwanja wa ndege.
Rais wa Palestina aomba kufanyika kwa mkutano utakaoishinikiza Israel kuondoka ardhi ya Palestina

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas Rais wa Palestina ametoa wito wa kufanyika kwa mkutano wa kimataifa wa amani ili kuhakikisha Israel inaondoka katika maeneo ya Palestina.
Rais wa Palestina Mahmoud Abbas alitoa wito wa ulazima wa kufanyika mkutano wa kimataifa wa amani ili kuhakikisha Israel inajiondoa katika maeneo ya Palestina "kulingana na maazimio ya uhalali wa kimataifa na ratiba maalum."
Abbas aliongeza, wakati wa mkutano wake na mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Mchakato wa Amani ya Mashariki ya Kati, Tor Wensland, kwamba juhudi lazima ziunganishwe ili kuzuia kuhama kwa Mpalestina yeyote, iwe kutoka Ukanda wa Gaza au Ukingo wa Magharibi, ikiwa ni pamoja na Jerusalem Mashariki, kusimamisha mashambulio yote, na kuachilia fedha za Wapalestina kwa ukamilifu, kulingana na taarifa. Imechapishwa na rais wa Palestina kwenye Facebook.
Rais huyo wa Palestina alisisitiza "umuhimu wa kuiwezesha nchi ya Palestina kisiasa na kiuchumi ili iweze kutekeleza kikamilifu majukumu yake kwa wananchi wa Palestina huko Jerusalem, Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan," akimtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, "kuendeleza juhudi zake na kuzidisha juhudi za Umoja wa Mataifa ili kukomesha uchokozi unaoendelea wa Israel dhidi ya watu wa Palestina, na kuhakikisha ongezeko la misaada ya kibinadamu na misaada ya vifaa vya makazi kwa wakazi wa ukanda wa Gaza, haswa katika hali mbaya ya hali ya hewa ya sasa
Tuzo za Grammy 2024: Taylor Swift aweka historia kwa kushinda tuzo ya albamu bora

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Taylor Swift Taylor Swift alitawala maonyesho ya Tuzo za Grammy za mwaka huu, kwa kuwa msanii wa kwanza kushinda tuzo ya albamu ya mwaka mara nne.
Nyota huyo hapo awali alikuwa ameshinda tuzo tatu za albamu bora akiwa na Stevie Wonder, Paul Simon na Frank Sinatra.
Alipokea tuzo kutoka kwa Celine Dion, ambaye alionekana kwa kushtukiza . Swift pia alitumia tukio hilo kutoa albamu yake mpya iliowashangaza wengi.
Miley Cyrus na Billie Eilish walitwaa tuzo nyingine bora katika sherehe za Jumapili.
Mchango wa Eilish kwenye wimbo wa filamu ya Barbie, What Was I Made For?, ulishinda wimbo bora wa mwaka, akiishinda Anti-Hero ya Swift pamoja na nyimbo za SZA, Cyrus na Olivia Rodrigo.
"Kila mtu katika kitengo hiki - ilikuwa orodha ya watu wenye vipawa vya ajabu, wasanii wa ajabu, muziki wa ajabu. Nasikia furaha sasa hivi."
Wimbo huo pia ulishinda wimbo bora zaidi ulioandikwa kwa vyombo vya Habari vinavyotumia video, huku albamu ya Barbie - ambayo iliwekwa pamoja na mtayarishaji Mark Ronson - iikishinda tuzo ya wimbo bora wa mkusanyo wa vyombo vya habari vya kuona.
Tazama: Marekani yarusha makombora kuwalenga Wahouthi kutoka katika meli ya kivita
Maelezo ya video, Marekani yarusha makombora kuwalenga Wahouthi kutoka katika veli ya kivita Moto wa msitu Chile: Takriban watu 112 wamekufa katika eneo la Valparaiso

Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/SHUTTERSTOCK
Takriban watu 112 wameuawa na moto wa misitu katika mkoa wa Valparaiso nchini Chile, mamlaka za eneo zimesema.
Gabriel Boric alitangaza hali ya hatari na kusema atatoa "rasilimali zote muhimu" ili kukabiliana na hali hiyo.
Inaaminika kuwa moto mbaya zaidi wa msitu wa Chile kuwahi kurekodiwa. Wengi wa walioathiriwa walikuwa wakizuru eneo la pwani wakati wa likizo za majira ya joto.
Tahadhari ya afya iliwekwa mjini Valparaiso na wizara ya afya.
Wanafunzi wa udaktari wanaokaribia kumaliza masomo yao wataajiriwa ili kusaidia kupunguza shinikizo kwa huduma ya afya, wizara ilitangaza katika taarifa hiyo hiyo.
Huduma za uokoaji zimetatizika kufikia maeneo yaliyoathirika zaidi na Waziri wa Mambo ya Ndani Carolina Tohá alisema idadi ya waliofariki "itafikia idadi kubwa zaidi" katika saa zijazo.
Serikali ya Chile imewataka watu kutosafiri kwenda katika maeneo yaliyokumbwa na moto huo.
Marekani yaendeleza mashambulizi zaidi dhidi ya wapiganaji wa Houthi nchini Yemen

Chanzo cha picha, EPA
Marekani imefanya mashambulizi zaidi dhidi ya makombora ya Houthi nchini Yemen siku ya Jumapili, afisi Kuu ya Marekani (Centcom) ilisema katika taarifa kwenye X.
Centcom ilisema vikosi vya Marekani vilishambulia kombora la ardhini na makombora manne ya kuzuia meli ambayo "yalitayarishwa kurushwa dhidi ya meli katika Bahari ya shamu".
Hatua ya hivi punde zaidi ya kijeshi inakuja siku moja baada ya Marekani na Uingereza kushambulia maeneo yanayolengwa na Wahouthi.
Hii inafuatia kuendelea kwa mashambulizi ya kundi hilo la Yemeni linaloungwa mkono na Iran dhidi ya meli za kijeshi na zile za mizigo katika Bahari ya shamu.
Mashambulizi ya Houthi yamelazimu makampuni makubwa ya meli kuepuka njia ya maji, na kuathiri biashara ya kimataifa.
Misri imesema mapato yake kutoka kwa Mfereji wa Suez yalipungua kwa karibu nusu mwezi Januari, huku idadi ya meli zinazosafiri kupitia njia muhimu ya biashara mwezi uliopita ikipungua kwa zaidi ya theluthi.
Mashambulizi ya pamoja ya Marekani na Uingereza ya Jumamosi yalipamba anga la usiku kusini mwa mji mkuu wa Yemen wa Sana'a, huku mwanaharakati mmoja wa haki za binadamu na mkazi wa eneo hilo akiambia BBC kuwa nyumba zinatetemeka.
Maafisa wa Houthi walikaidi kujibu mashambulizi yaliyoongozwa na Marekani - na kuapa kujibu.
Akijibu mashambulio ya Jumamosi, msemaji wa jeshi la kundi hilo, Yahya Sarea, aliandika kwenye X: "Mashambulizi haya hayatatuzuia kutoka kwa msimamo wetu wa kiadili, kidini na wa kibinadamu wa kuunga mkono watu wa Palestina walio na uthabiti katika Ukanda wa Gaza na hayatapita bila jibu au bila kuadhibiwa."
Natumai hujambo

