Mauaji ya wanawake Kenya: Mamia waandamana kupinga ukatili dhidi ya wanawake

Chanzo cha picha, Mercy Juma BBC
Maandamano yanafanyika katika miji mikuu nchini Kenya kupinga ongezeko la visa vya mauaji ya wanawake na unyanyasaji mwingine dhidi ya wanawake.
Mamia wamekusanyika Nairobi, Nakuru, Mombasa, Nyeri na Lodwar, wengine wakiwa wamebeba mabango yenye majina ya waliouawa.Utafiti wa 2022 uligundua angalau mwanamke mmoja kati ya watatu wa Kenya alivumilia unyanyasaji wa kimwili wakati fulani maishani mwao."
Niko hapa kwa sababu nina hasira," Winnie Chelagat mwenye umri wa miaka 33 aliambia BBC."Ni makosa, tumechoka na tunataka kitu kifanyike kuhusu hilo.
"Wanaume na wavulana lazima wawajibike kwa matendo yao wenyewe badala ya mzigo kuwa kwa wanawake na wasichana kujilinda, alisema mwandamanaji mwingine anayeitwa Michael Onyango.
"Tunapaswa kuwaelimisha watoto wetu wa kiume na kuwaambia kwamba wanahitaji kuacha kuua wanawake.
"Maandamano ya Jumamosi yanafuatia mfululizo wa mauaji ya kutisha ya wanawake - ikiwa ni pamoja na mwathiriwa mmoja, ambaye baadaye aliitwa Rita Waeni, ambaye mabaki yake yaliyokatwakatwa yalipatikana yakiwa yameingizwa kwenye mfuko wa plastiki katika nyumba ya kukodisha ya Airbnb.
Uuaji wa wanawake unafafanuliwa kuwa kuua kwa makusudi mwanamke au msichana kwa sababu wao ni wa kike.
Shirika la Amnesty International linasema zaidi ya visa 500 vya mauaji ya wanawake vilirekodiwa nchini Kenya kati ya mwaka wa 2016 na 2023.
Wengi wa wahasiriwa waliuawa na washirika wa karibu au watu wanaojulikana.
Wanaharakati wanataka mamlaka kuharakisha haki kwa waathiriwa wote wa hivi majuzi wa unyanyasaji wa kingono na kijinsia.
Makumi ya makundi ya haki za mitaa yanasema kuwa serikali lazima itangaze mauaji ya wanawake kuwa dharula ya kitaifa na mauaji ya tabaka kama uhalifu mahususi, tofauti na mauaji.
Jijini Nairobi siku ya Jumamosi, waandamanaji waliimba "Sisi ni watu sio wanyama" kwa Kiswahili - wakimaanisha "sisi ni binadamu si wanyama".
Wengine walibeba mabango yanayosema "wanaume dhaifu tu ndio wanaoua wanawake" na "kila unapomlaumu mwathiriwa unathibitisha muuaji".
Kushutumu waathiriwa kumeenea kwenye mitandao ya kijamii, huku watoa maoni katika kile kinachoitwa "manosphere" nchini Kenya wakiwalaumu wanawake waliouawa kwa vifo vyao wenyewe.
Jumbe nyingi kwenye majukwaa ya mtandaoni huzingatia kile waathiriwa walikuwa wamevaa waliposhambuliwa, au huhoji kwa nini hawakutumia simu zao za rununu kuwaambia familia na marafiki waliko.
Licha ya Kenya kuwa na sheria thabiti dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia, wahalifu wengi hawaadhibiwi.
Mashtaka yanapoletwa, mara nyingi husonga mbele kwa miaka mingi mahakamani.


