Biden asema amewasilisha ujumbe wa faragha kwa Iran kuhusu mashambulizi ya Houthi

Taarifa kutoka Washington hivi punde zinasema Rais Joe Biden anasema Marekani imewasilisha ujumbe wa faragha kwa Iran kuhusu Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena hapo kesho.

  2. Biden asema amewasilisha ujumbe wa faragha kwa Iran kuhusu mashambulizi ya Houthi

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Taarifa kutoka Washington hivi punde zinasema Rais Joe Biden anasema Marekani imewasilisha ujumbe wa faragha kwa Iran kuhusu Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran waliohusika katika kuzishambulia meli za kibiashara katika Bahari ya Shamu, shirika la habari la Reuters linaripoti.

    "Tuliiwasilisha kwa faragha na tuna imani kuwa tumejiandaa vyema," Biden aliwaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House.

    Soma zaidi:

    • Tunachojua kuhusu shambulio dhidi ya Wahouthi na mkakati nyuma yake
    • Wahouthi ni nani na kwa nini wanashambulia meli zinazopita Bahari ya Shamu?
  3. Serikali ya Yemen yawalaani Wahouthi kwa 'kuzidisha' mivutano

    h

    Yemen imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka mingi - huku Wahouthi wakidhibiti sehemu kubwa ya magharibi mwa Yemen, ukiwemo mji mkuu Sanaa.

    Sasa, serikali ya Yemen inayotambuliwa kimataifa imewalaani Wahouthi kwa "kuingiza nchi kwenye mzozo" baada ya mashambulizi ya Marekani na Uingereza yaliyowalenga Wahouthi wiki hii.

    Katika taarifa, iliyoshirikiwa na shirika rasmi la habari la Saba siku ya Ijumaa, mamlaka yenye makao yake mjini Aden imewashutumu waasi kwa "kuanzisha mzozo wa propaganda", kufuatia mashambulizi yao dhidi ya meli za wafanyabiashara katika Bahari ya Sahamu, na "madai ya uongo" ya kuiunga mkono Gaza.

    Ilisisitiza juu ya haja ya kurejesha taasisi halali za serikali nchini Yemen ili kuhakikisha usalama katika Bahari Shamu unaimarika.

    Serikali pia ililaani mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza na kutoa wito wa upatikanaji wa haraka wa misaada ya kibinadamu kwa Wapalestina.

  4. Maelfu ya watu washiriki maandamano ya wafuasi wa Palestina London

    g
    Maelezo ya picha, Waandamanaji wakiwa na sanamu ya "Little Amal ".

    Maelfu ya watu wanashiriki maandamano makubwa ya kwanza ya mwaka mpya kuwaunga mkono watu wa Palestina.

    Waandalizi wanasema maandamano hayo ni sehemu ya siku ya kimataifa ya utekelezaji inayoshirikisha nchi 30. Wanatoa wito wa kusitishwa kamili wa mapigano

    Gaza - mengi ya mabango yana ujumbe ulioandikwa"Sitisha mapigano Sasa!"

    Tumeona sanamu kubwa ya kutengenezwa ya mtoto mkimbizi wa Syria anayeitwa Little Amal, ambaye atatembea na waandamanaji kwa lengo la kuwaangazia watoto wakimbizi.

    Kuna uwepo mkubwa wa polisi na karibu maafisa 1,700 wako kazini. Haya ni maandamano ya saba ya kitaifa na polisi mjini London wanasema maandamano mengi yamefanyika bila ghasia, lakini kumekuwa na watu kadhaa waliokamatwa.

    Afisa anayeongoza oparesheni hiyo - Naibu Kamishna Msaidizi Laurence Taylor - anasema mtu yeyote ambaye "kwa makusudi anawalazimisha polisi kuchukua hatua" kwenye mabango na kauli mbiu anaonywa kwamba atakamatwa.

    g

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Maandamano yanafanyika duniani kote - picha hii ilipigwa nje ya Ubalozi mdogo wa Marekani mjini Johannesburg, Afrika Kusini

    oma zaidi:

    • Maafisa wa Israel wanataka kuiangamiza Gaza- Mahakama ya ICJ yafahamishwa
    • Kuna wakimbizi wangapi wa Kipalestina duniani kote
    • Silaha nne ambazo Hamas inazitumia kupigana na Israel
  5. Israel yasitisha mapigano mjini Rafah huku wakaazi wakielezea mashambulizi 'yasiyofikirika''

    f

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Picha hii iliyopigwa Rafah tarehe 10 Januari inaonyesha uharibifu kufuatia mashambulio ya Israeli

    Mjini Gaza Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) limetangaza ‘’kusimamishwa kwa shughuli za kijeshi kwa muda’’kwa madhumuni ya kibinadamu" mjini Rafah hadi nane za mchana kwa saa za eneo.

    Hatua hii inafuatia usiku wa mashambulizi ya Israeli katika mji wa kusini, ambapo watu wengi kutoka mahali maeneo mbali mbali ya Gaza wamekimbilia.

    Samir Qeshta anasema nyumba yake "iliharibiwa kabisa" katika shambulio hilo.

    "Nyumba hii ilinihifadhi mimi na watoto wangu. Nilikuwa nikijiandaa kwa ajili ya mwanangu wa kiume kuoa ndani yake, nilikuwa nimeipaka rangi," aliambia shirika la habari la AFP.

    "Sisi ni watu wa amani, walitupiga bila tahadhari. Nilikuwa nikimtembelea dada yangu na mke wangu alikuwa nyumbani kwa wazazi wake."

    Nimma al-Akhras alikuwa nyumbani wakati mashambulizi ya mabomu yalipoanza.

    "Mashambulizi yalikuwa sio ya kufikirika," anasema. “Tulianza kupiga kelele na sikuweza kusogea hadi mtu akanibeba na kuniweka kwenye mkokoteni.

    "Tumekosea nini? Tulikuwa tumekaa tu. Si salama majumbani mwetu wala nje, sijui twende wapi?"

    Israel inasema inawalenga magaidi na miundombinu yao - na kwamba inajaribu kupunguza vifo vya raia.

    h

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Mwanzoni mwa mzozo , watu wengi wa Gaza walilazimika kukimbia makazi yao kaskazini na kutafuta makazi Rafah - picha hii ilipigwa siku ya Alhamisi.

    Soma zaidi:

    • Maafisa wa Israel wanataka kuiangamiza Gaza- Mahakama ya ICJ yafahamishwa
    • Kuna wakimbizi wangapi wa Kipalestina duniani kote
    • Silaha nne ambazo Hamas inazitumia kupigana na Israel
  6. Uturuki yashambulia maeneo 29 ​​ndani ya Iraq na Syria

    h

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan(pichani) akizungumza wikendi iliyopita

    Wizara ya ulinzi ya Uturuki imesema imefanya mashambulizi ya anga usiku kucha dhidi ya "eneo la magaidi" katika nchi za Iraq na Syria baada ya wanajeshi wake tisa kuuawa katika kambi ya kijeshi nchini Iraq.

    Inasema kuwa mashambulizi hayo yalilenga maeneo 29 ​​yakiwemo "mapango, mahandaki, makazi na mitambo ya mafuta" ya chama cha Kurdistan Workers' Party (PKK) na wanamgambo wa Kitengo cha Ulinzi wa Watu (YPG) – ambao Uturuki inayaona kama makundi ya kigaidi.

    Uturuki imekuwa na harakati za muda mrefu za jijeshi dhidi ya PKK, kundi ambalo pia linatambuliwa na nchi nyingi za Magharibi - ikiwa ni pamoja na Uingereza na Marekani - kama shirika la kigaidi.

  7. Habari za hivi punde, William Lai atarajiwa kuwa rais ajaye wa Taiwan baada ya upinzani kukubali

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    William Lai anatarajiwa kuwa rais ajaye wa Taiwan baada ya upinzani kukubali kushindwa.

    Hou Yu-ih na mgombea mwenza wake Jaw Shau-king wamekubali kushindwa kwenye mkutano wa chama chake cha KMT mjini Taipei: "Asanteni nyote. Nilijaribu niwezavyo, nina huzuni sana kwamba sikuweza kukamilisha mabadiliko ya serikali. Samahani sana," alisema Hou Yu-ih wa KMT.

    Bw Lai kutoka chama cha DPP amekuwa mgombea urais wa kwanza kupata kura milioni tano, kulingana na vituo vya utangazaji vya ndani.

    Kura zimehesabiwa kutoka zaidi ya 90% ya vituo vya kupigia kura kote Taiwan, kulingana na taarifa za moja kwa moja zilizotolewa na Tume ya Kati ya Uchaguzi.

    Kwanini uchaguzi wa Taiwan ni umuhimu kwa ulimwengu?

    Rais ajaye wa Taiwan atatengeneza uhusiano na Beijing na Washington. Kisiwa hiki ni kielelezo muhimu katika mzozo wao wa kugombea madaraka katika eneo hili.

    Beijing imekuwa ikidai kisiwa hicho kwa muda mrefu, lakini uhusiano umedorora sana katika miaka ya hivi karibuni chini ya Rais Tsai Ing-wen na Chama cha Maendeleo cha Kidemokrasia (CMK).

    Uchina imeongeza shinikizo la kijeshi kwenye kisiwa hicho katika mwaka uliopita na idadi ya rekodi ya uvamizi.

    Kuongezeka kwa mzozo wa aina yoyote kati ya Uchina na Taiwan kuna hatari ya kugeuka kuwa kitu kikubwa na hatari zaidi.

    Marekani ina jeshi kubwa la wanamaji katika eneo hilo, wakati Australia na Japan pia zikiwa na ngome karibu na kisiwa hicho.

    Vita nchini Taiwan vitakuwa vya kuangamiza watu wote na kama pigo kwa demokrasia ya kisiwa hicho.

    Pia vita vitadhoofisha uchumi wa dunia. Karibu nusu ya meli za shehena za mizigo duniani hupitia Mlango-Bahari wa Taiwan kila mwaka, na kuifanya kuwa kitovu muhimu kwa biashara ya kimataifa.

  8. Tazama: Mkongwe wa miaka 102 akisherehekea siku ya kuzaliwa kwenye uwanja wa barafu

    Maelezo ya video, Tazama: Nyama wa 102- akisherehekea siku ya kuzaliwa kwenye uga wa mchezo wa kuteleza kwenye theruji wa Dorset

    Bibi mmoja alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 102 kwa kuteleza kwenye barafu kwa mara ya kwanza tangu alipokuwa msichana.

    Eileen Pickering aliingia uwanjani Bournemouth baada ya wafanyikazi wa nyumba yake ya uangalizi kupanga tukio hilo.

    Alianza kuteleza kwenye barafu baada ya mechi za hoki ya barafu kwenye uwanja wake wa karibu huko London alipokuwa msichana mdogo lakini hakuweza kupata ukumbi kucheza mchezo huo alioupenda wakati familia yake ilipohamia Dorset.

    Nyanya huyo alisema kucheza kwake tena mchezo wa kuteleza kwenye theluji kulimfanya ajihisi kama "ndoto iliyotimia".

  9. Habari za hivi punde, Vita vya Gaza: Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas inasema watu wengine 135 wameuawa Gaza

    Kama tumekuwa tukiripoti, mashambulizi katika Bahari ya Shamu naYemen yanahusishwa na vita vya Israeli dhidi ya Gaza.

    Na, katika taarifa yake , wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas mjini Gaza inasema kuwa watu 23,843 wameuawa huko tangu tarehe 7 Oktoba.

    Hilo ni ongezeko la watu 135 kwa jumla kulingana na idadi iliyotolewa Ijumaa.

    Wizara pia inasema imesajili majeruhi 60,317

    Soma zaidi:

    • Maafisa wa Israel wanataka kuiangamiza Gaza- Mahakama ya ICJ yafahamishwa
    • Kuna wakimbizi wangapi wa Kipalestina duniani kote
    • Silaha nne ambazo Hamas inazitumia kupigana na Israel
    f

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, h
  10. Habari za hivi punde, Wahouthi waapa 'kujibu kwa ufanisi' shambulio la hivi punde la Marekani

    Afisa kutoka ofisi yake ya kisiasa ya Ansarullah ya Wahouthi ameiambia televisheni ya Al Jazeera, kupitia Reuters, kuwa hakukuwa na majeraha katika shambulio la hivi punde la Marekani dhidi ya Yemen.

    Afisa huyo pia anaapa kuwa kutakuwa na "jibu kali na la ufanisi" dhidi ya shambulio la usiku kutoka kwa marekani.

    Wakati huo huo Msemaji wa waasi wa Houthi ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba mashambulizi ya hivi majuzi ya Marekani na Uingereza dhidi ya Yemen - ikiwa ni pamoja na shambulio la jana usiku - "hayakufanikiwa".

  11. Waziri wa mambo ya nje wa Iran aunga mkono mashambulizi ya Wahouthi katika Bahari ya Shamu

    h

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kama tulivyoripoti hapo awali, Iran inaunga mkono Houthis nchini Yemen - na Marekani inaamini kuwa Iran "inahusika sana" katika kupanga mashambulizi ya Houthi dhidi ya meli za mizigo katika Bahari ya Shamu.

    Kwa kuzingatia hilo, labda haishangazi kwamba waziri wa mambo ya nje wa Iran amesifu hatua za Houthi "dhidi ya Israeli" katika Bahari ya Shamu, na kuongeza kuwa Yemen "imejitolea kwa usalama wa baharini na meli".

    Kwenye chapisho lake la X jana Ijumaa, Hossein Amir-Abdollahian alisema: "Hatua ya Yemen ya kuwaunga mkono wanawake na watoto wa Gaza na upinzani wake dhidi ya mauaji ya kimbari ya utawala wa Israel ni ya kupongezwa."

    Pia aliitaka Marekani "ikomeshe mara moja" uungaji mkono wake kwa Israel - badala ya kuanzisha mashambulizi dhidi ya Yemen - "ili usalama urejee katika eneo zima".

  12. Vita vinaendelea Gaza huku Marekani ikiwashambulia waasi wa Houthi nchini Yemen

    h

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Wapalestina wakiwabeba ndugu waliojeruhiwa kwenye machela katika mji wa Gaza

    Wapalestina wakiwa wamebeba ndugu waliojeruhiwa kwenye machela katika mji wa Gaza

    Wahouthi wanasema wanalenga meli katika Bahari ya Shamu zinazomilikiwa au zinazoelekea Israel, ili kuonyesha uungaji mkono wao kwa Hamas huko Gaza. Sawa na Wahouthi, Hamas wanaungwa mkono na Iran.

    Mjini Gaza, Wapalestina wamekabiliwa na usiku mwingine wa mashambulizi ya mabomu ya Israeli, na ripoti za mashambulizi zimeripotiwa katika Ukanda huo.

    • Katika taarifa yake ya asubuhi, Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) linasema liliharibu shimo la handaki, lililokuwa na vifaa vya vilipuzi, na kuwua "magaidi" kadhaa katika mji wa Khan Younis.
    • Shirika la habari la Palestina Wafa pia linaripoti mashambulizi katika mji wa Kaskazini mwa Gaza - huku watu 20 wakiripotiwa kuuawa.
    • Katika kitongoji cha Al-Dawa, kaskazini mwa Nuseirat katikati mwa Gaza,watu "kumi na wawili" waliripotiwa kuuawa, inasema Wafa.
    • IDF inasema iligundua na kuharibu majengo mawili ya kurushia roketi katika eneo la Al Mu'araqaka tikati mwa Gaza
    • Katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu , Wapalestina watatu waliuawa katika kile ambacho majeshi ya Israel yanakiita kuwaangamiza "magaidi" waliojipenyeza kwenye makazi ya Waisraeli ya Adorana kushambulia vikosi vya Israel.
    • Siku ya Ijumaa usiku, makombora yalirushwa kuelekea kusini mwa Israel kutoka Gaza
    • Na katika mpaka wa kaskazini na Lebanon, IDF inaripoti ubadilishanaji wa risasi Jumamosi asubuhi. Jeshi la anga la Israeli liliharibu miundombinu ya "kigaidi", inaongeza

    Soma zaidi:

    • Maafisa wa Israel wanataka kuiangamiza Gaza- Mahakama ya ICJ yafahamishwa
    • Kuna wakimbizi wangapi wa Kipalestina duniani kote
    • Silaha nne ambazo Hamas inazitumia kupigana na Israel
  13. Mashambulio ya Marekani dhidi ya Wahouthi: Makombora ya Tomahawk ni nini?

    h

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Kombora la Tomahawk likifyatuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2018

    Shambulio la hivi punde kwenye eneo la rada nchini Yemen lilitekelezwa kwa makombora ya Tomahawk.

    Lakini je Tomahawk ni nini?

    Tomahawks ni makombora ya mashambulio ya ardhini ambayo yanaongozwa na GPS na yanaweza kuratibiwa kuruka kwa kukwepa, jeshi la Marekani linasema.

    Ni makombora ya masafa marefu na hutumiwa kimsingi na Jeshi la Wanamaji la Marekani na jeshi la Wanamaji la Uingereza katika shughuli za uvamizi wa meli na nyambizi.

    Yametengenezwa kuwa na uwezo wa kuruka katika mwinuko wa juu sana kwa kasi ndogo ndogo, kulingana na Amri ya Mifumo ya Anga ya Wanamaji ya Marekani.

    Marekani iliyatumia kwa mara ya kwanza makombora ya Tomawsk wakati wa Operesheni ya Dhoruba ya Jangwa katika Vita vya Ghuba mnamo 1991.

    Soma zaidi:

    • Tunachojua kuhusu shambulio dhidi ya Wahouthi na mkakati nyuma yake
    • Wahouthi ni nani na kwa nini wanashambulia meli zinazopita Bahari ya Shamu?
  14. Marekani yafanya shambulio jipya la makombora dhidi ya maeneo ya wahouthi

    h

    Karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja, baada ya shambulio jipya la Marekani lililowalenga Wahouthi nchini Yemen saa za mapema Jumamosi asubuhi.

    • Shambulio hilo lililenga maeneo ya rad ana makombora ya Tomahawkyaliyorushwa kutoka kwenye meli, jeshi la Marekani limesema.
    • Hatua hii ya hivi punde ya Marekani inajiri baada ya waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran kuonya kuwa watafanya mashambulizi zaidi kwenye meli katika Bahari ya Shamu.
    • Mashambulizi ya Jumamosi asubuhi ya Marekani yanafuatia mashambulio yaliyoratibiwa ya Marekani na Uingereza Alhamisi usiku, wakati maeneo karibu 30 yanayodhibitiwa na Wahouthi yalipopigwa.
    • Kiongozi wa Houthis aliapa kulipiza kisasi kwa Uingereza na Marekani
    • Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa wito kwa pande zote " kusitisha mashambulizi

    Soma zaidi:

    • Tunachojua kuhusu shambulio dhidi ya Wahouthi na mkakati nyuma yake
    • Wahouthi ni nani na kwa nini wanashambulia meli zinazopita Bahari ya Shamu?
  15. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja leo ikiwa ni tarehe 13.01.2024