Shirika la msalaba mwekundu la Palestina lasema watoto waliozaliwa kabla ya wakati wamehamishwa kutoka al-Shifa

Shirika la Msalaba mwekundu la Palestina (PCRS) linasema lilifanikiwa kuwahamisha watoto 31 wanaozaliwa kabla ya wakati kutoka hospitali ya al-Shifa siku ya Jumapili.

Moja kwa moja

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena hapo kesho majaaliwa.

  2. Wanajeshi wa Israel wawateka Wapalestina 70 katika Ukingo wa Magharibi

    h

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Mwanamume akikagua uharibifu ndani ya nyumba iliyoteketea, kufuatia uvamizi wa Israel kwenye kambi ya wakimbizi ya Balata, mashariki mwa mji wa Nablus katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, tarehe 19 Novemba, 2023

    Vikosi vya Israel viliwakamata Wapalestina 70 usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili wakiwemo wanawake 3 na waandishi wa habari 2, kutoka Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, kulingana na Klabu ya Wafungwa wa Palestina.

    Ilisema kuwa kukamatwa kwa watu hao kulijiri kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi, katika kambi za Balata na Jenin.

    Idadi ya waliokamatwa katika Ukingo wa Magharibi tangu Oktoba 7 imeongezeka hadi watu 2,920 hadi sasa.

    Vita vya Gaza: Mengi zaidi

    • Je Israel inapanga kushambulia vipi mahandaki ya Hamas?Hezbollah yaonya vita vya kikanda ikiwa mashambulizi Gaza yataendelea
    • Mtoto mmoja huuawa kila baada ya dakika kumi Gaza
    • Nchi ya Amerika Kusini ambayo ina jamii kubwa zaidi ya Wapalestina nje ya Ulimwengu wa Kiarabu na Israeli
    • 'Ninapiga simu kutoka shirika la ujasusi la Israel.Tunarusha bomu, una saa mbili kuondoka’
    • Vita vya Israel na Gaza: Je, uhalifu wa kivita unatekelezwa?, sheria inasemaje?
  3. Shirika la msalaba mwekundu la Palestina lasema watoto waliozaliwa kabla ya wakati wamehamishwa kutoka al-Shifa

    g

    Chanzo cha picha, PCR

    Maelezo ya picha, Shirika hilo lilichapisha picha za ambulensi kwenye X, ambayo inasema ilisafirisha watoto hao

    Shirika la Msalaba mwekundu la Palestina (PCRS) linasema lilifanikiwa kuwahamisha watoto 31 wanaozaliwa kabla ya wakati kutoka hospitali ya al-Shifa siku ya Jumapili.

    Walihamasishwa kwa uratibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu.

    WHO ilitoa taarifa mapema ikisema kulikuwa na wagonjwa 291 ambao bado wako hospitalini - wakiwemo watoto 32 waliozaliwa kabla ya wakati.

    Bado haijabainika kwa nini idadi ya watoto wanaotolewa na PCRS na WHO ni tofauti, na BBC haiwezi kuthibitisha takwimu hizi kwa kujitegemea.

    Kama tulivyoripoti jana, mamia ya watu wameondoka katika hospitali kubwa zaidi ya Mji wa Gaza, al-Shifa, katika siku chache tangu jeshi la Israel liingie kwenye jengo hilo kutekeleza kile walichokiita "operesheni sahihi dhidi ya Hamas".

  4. Andre Onana: Kipa wa Manchester United ajeruhiwa akiichezea Cameroon

    .
    Maelezo ya picha, Kipa Andre Onana

    Kipa Andre Onana atarejea Manchester United kugundua ukubwa wa jeraha alilopata akiichezea Cameroon katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia.

    Onana, 27, alibadilishwa dakika ya 81 katika ushindi wa 3-0 wa Ijumaa dhidi ya Mauritius mjini Douala, baada ya kuumia akiokoa.

    Kipa huyo amejiondoa kwenye kikosi cha Cameroon kitakachocheza Jumanne dhidi ya Libya.

    Maafisa wa Cameroon hawakutoa maelezo kuhusu ukubwa wa jeraha hilo.

    Onana, aliyesajiliwa kutoka Inter Milan kwa pauni milioni 47.2 mwezi Julai, amecheza mechi zote 18 za mashindano za United kufikia sasa msimu huu.

    Meneja wa United Erik ten Hag tayari anakabiliwa na matatizo kadhaa ya majeruhi wakati kikosi chake kikijiandaa kurejea kutoka kwa mapumziko ya kimataifa na Ligi ya Premia dhidi ya Everton mnamo 26 Novemba na ziara ya Ligi ya Mabingwa huko Galatasaray siku tatu baadaye.

    Majeraha ya Man United

    Lisandro Martinez (mguu), Casemiro (paja) na Christian Eriksen (goti) wote wako nje huku Luke Shaw (shida ya misuli), Jonny Evans (paja), Tyrell Malacia (goti), Aaron Wan-Bissaka (mgonjwa) na Rasmus Hojlund. (paja) .

  5. Uchaguzi DRC 2023: Kampeni rasmi za uchaguzi wa urais zaanza

    g

    Chanzo cha picha, BBC/Mbelechi Msochi

    Maelezo ya picha, Rais wa sasa wa DRC Félix Tshisekedi, ambaye ni miongoni mwa wagombea 26 wa kiti cha urais

    Kampeni za uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi wa rais na wabunge zimeanza rasmi kote katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo leo Jumapili.

    Uchaguzi nchini hmo umepangwakufanyika Desemba 20, huku jumla ya wagombe 26 wakiwania kiti cha urais, akiwemo rais wa sasa Félix Tshisekedi.

    Atakabiliana na viongozi kadhaa wa upinzani ikiwa ni pamoja na Martin Fayulu, mgombea ambaye hakufanikiwa katika uchaguzi wa rais wa 2018, mfanyabiashara tajiri Moïse Katumbi, aliyekuwa gavana wa Katanga (kusini-mashariki) pamoja na Dkt Denis Mukwege, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel 2018 kwa juhudi zake za kuunga kuwahudumiwa wanawake waliobakwa.

    Wakazi wa mji mkuu Kinshasa na maeneo mengine wamejitokeza kushiriki kampeni za uchaguzi kunadi sifa na sera za wagombea wao:

    Hizi ni baadhi ya picha za kampeni ya uchaguzi kutoka mji mkuu wa Kinshasa

    h

    Chanzo cha picha, BBC / Mbelechi

    Maelezo ya picha, Rais walionekana wakiwa wamevalia mavazi mbali mbali yanayonadi sera na picha za wagombea wao
    g

    Chanzo cha picha, BBC/BBC Mbelechi Msochi

    Maelezo ya picha, Mabango ya picha za wagombea wa urais katika mji mkuu yameshuhudiwa katika maeneo mbali mbali ya mji mkuu Kinshasa
    g

    Chanzo cha picha, BBC /mbelechi Msochi

    g

    Chanzo cha picha, BBC/Mbelechi Msochi

  6. Marekani yaweka vikwazo kwa wanamgambo wa Kishia wa Iraq kwa "kuhusika" kwao katika mashambulizi dhidi ya Washington.

    f

    Chanzo cha picha, AFP

    Marekani imeviwekea vikwazo vikosi vya Hezbollah vya Iraq na wanamgambo wengine wa Kishia wanaoungwa mkono na Iran na washirika wake, ikiwatuhumu kuhusika na mashambulizi dhidi ya Marekani na washirika wake nchini Iraq na Syria.

    Marekani imeilaumu Iran na makundi yenye silaha inayoyaunga mkono kwa kuunga mkono mashambulizi zaidi ya 60 tangu katikati ya mwezi wa Oktoba, wakati ambapo mivutano ya kikanda inaongezeka kutokana na vita dhidi ya Gaza, vilivyoanza tarehe saba mwezi uliopita, wakati kundi la Hamas lilipoanzisha shambulio la kushtukiza katika miji ya Gaza.

    Takriban wanajeshi 59 wa Marekani walijeruhiwa wakati wa mashambulizi hayo, lakini wote walirejea kazini.

    Katika taarifa kwenye tovuti ya Telegram, Abu Ali Al-Askari, afisa wa usalama katika Brigedi ya Hezbollah ya Iraq, alielezea vikwazo hivyo kuwa "kichekesho," akiongeza kuwa hatua hizi "hazitaathiri" operesheni zinazofanywa na vikosi hivyo.

  7. Vita vya Ukraine: Zaidi ya makazi 150 yalipigwa makombora nchini Ukraine katika vita vya usiku kucha

    k

    Chanzo cha picha, Global Images Ukraine

    Warusi walirusha makombora matano na mashambulio 76 ya anga ndani ya Ukraine, na kufanya mashambulio 50 kutoka kwenye mifumo mingi ya kurusha roketi kwenye maeneo ya wanajeshi wa Ukraine na maeneo mengine yanayokaliwa na watu wengi, amesema Mkuu wa majeshi wa Ukraine.

    Zaidi ya makazi 150 katika mikoa ya Chernigov, Sumy, Kharkov, Lugansk, Donetsk, Zaporozhye, Kherson na Nikolaev yalichomwa moto.

    "Katika saa 24 zilizopita, mapigano 71 ya kijeshi yalitokea kufuatia shambulio la kigaidi la Urusi, kwa bahati mbaya, kuna vifo na majeruhi miongoni mwa raia. Majengo ya makazi ya kibinafsi na miundombinu mingine ya kiraia iliharibiwa na kuharibiwa," Anasema mkuu wa majeshi wa Ukraine katika taarifa.

    Kulingana na ripoti hiyo hiyo, vikosi vya ulinzi wa anga vya Ukraine viliharibu ndege 15 za Urusi.

    Katika moja ya wilaya za mkoa wa Kiev, kituo cha miundombinu kiliharibiwa kwa sababu ya mashambulio ya usiku ya ndege zisizo na rubani za Urusi, huduma ya vyombo vya habari vya utawala wa kijeshi wa mkoa iliripoti.

    Mkuu wa utawala wa kijeshi wa jiji la Kiev, Sergei Popko, mnamo Jumapili usiku alitoa onyo la uvamizi wa anga katika mji mkuu wa Ukraine lilitangazwa mara kadhaa - jeshi la Urusi lilifanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani katika "makundi mengi", ambayo "yaliishambulia Kiev kwa mawimbi tofauti.

    Kulingana na taarifa za awali, hakuna majeruhi katika uvamizi huo

    Usiku na asubuhi, Warusi walishambulia wilaya nne za mkoa wa Sumy kwa na mizinga, utawala wa eneo hilo umeripoti.

    Katika saa 24 zilizopita, jeshi la Urusi lilifyatua risasi kwenye makazi ya mpaka na eneo la mapigano katika wilaya za Kharkov, Chuguevsky na Kupyansky za mkoa wa Kharkov , alisema Oleg Sinegubov, ulisema utawala wa Kyiv.

    Ndege moja isiyo na rubani ya Urusi ilidunguliwa katika eneo la Cherkasy , alisema mkuu Bw, Igor Taburets na kuongeza kuwa nyumba tano ziliharibiwa kidogo na hakuna watu waliojeruhiwa.

    Wanajeshi wa Urusi walifyatua makombora 389 katika eneo la Khersonkatika muda wa saa 24 zilizopita , na kuwajeruhi watu wanne, alisema mkuu wa utawala wa eneo hilo, Alexander Prokudin na kuongeza kuwa makombora hayo yaligonga maeneo ya kadhaa ya makazi ya watu katika mkoa huo na eneo lenye shughuli za biashara za kilimo.

    Vita vya Ukraine: Mengi zaidi:

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  8. Wapalestina 15 wauawa katika shambulio la Israel dhidi ya Khan Yunis na kambi ya Nuseirat katika Ukanda wa Gaza.

    g

    Chanzo cha picha, Ahmad Hasaballah/Getty Images

    Maelezo ya picha, Picha ya tarehe 13 Novemba 2023 ikionyesha Wapalestina waliojeruhiwa katika uvamizi wa Israel, wakiwasili katika Hospitali ya Nasser katika eneo la Khan Yunis katika Ukanda wa Gaza

    Shirika la Habari la Palestina (Wafa) limeripoti kuwa Wapalestina 15 wameuawa alfajiri ya Jumapili, katika shambulio la anga la Israel katikati na kusini mwa Ukanda wa Gaza.

    Shirika hilo limesema kuwa watu 13 waliuawa katika uvamizi wa Israel kwenye nyumba moja katika kambi ya Nuseirat, iliyopo katikati ya Ukanda wa Gaza, huku mwanamke mmoja na mtoto wake wakiuawa katika uvamizi mwingine uliotokea katika mji wa Khan Yunis, kusini mwa Gaza.

    Vita vya Gaza: Mengi zaidi

    • Je Israel inapanga kushambulia vipi mahandaki ya Hamas?Hezbollah yaonya vita vya kikanda ikiwa mashambulizi Gaza yataendelea
    • Mtoto mmoja huuawa kila baada ya dakika kumi Gaza
    • Nchi ya Amerika Kusini ambayo ina jamii kubwa zaidi ya Wapalestina nje ya Ulimwengu wa Kiarabu na Israeli
    • 'Ninapiga simu kutoka shirika la ujasusi la Israel.Tunarusha bomu, una saa mbili kuondoka’
    • Vita vya Israel na Gaza: Je, uhalifu wa kivita unatekelezwa?, sheria inasemaje?
  9. WHO inasema hospitali ya al-Shifa ya Gaza ni eneo la vifo, huku mamia wakiondoka

    h
    Maelezo ya picha, Wakimbizi wa Al-Shifa wanakimbia huku kukiwa na milio ya risasi, na mizinga ya jeshi la Israeli (IDF) ikiendelea

    Shirika la Afya Duniani (WHO) limeitaja hospitali ya al-Shifa katika mji wa Gaza kama "eneo la kifo" baada ya kutembelea hospitali hiyo.

    Timu ya pamoja ya Umoja wa Mataifa ikiongozwa na WHO iliikagua hospitali hiyo kwa muda wa saa moja kufuatia kukaliwa na jeshi la Israeli kuwaondoa wagonjwa na wahudumu wa afya na kuwahamishia kwingine.

    Timu hiyo ilisema iliona ushahidi wa milio ya risasi na kuona kaburi la pamoja kwenye lango la hospitali hiyo.

    Waliambiwa kuwa kaburi hilo lina miili ya watu 80.

    Kufuatia uhamishaji ambao mkurugenzi wa hospitali alisema uliamriwa na jeshi la Israel lakini ambao jeshi lilisema liliombwa na mkurugenzi, wagonjwa 300 waliokuwa mahututi wamesalia katika al-Shifa - hospitali kubwa na ya hali ya juu zaidi ya zamani mjini Gaza.

    WHO imesema inajaribu kupanga uhamishaji wa haraka wa wagonjwa waliosalia na wafanyakazi hadi vituo vingine vya afya mjii Gaza, na kutoa wito wa mara kwa mara wa kusitisha mapigano.

    Wakati huo huo, Ikulu ya Marekani imejibu ripoti gazeti la Washington Post iliyosema Israel, Hamas na Marekani ziko katika harakati za makubaliano ambayo yatahakikisha kuachiliwa kwa wanawake na watoto waliokamatwa na Hamas tarehe 7 Oktoba badala ya tano- mapumziko ya siku katika mapigano.

    Msemaji wa Ikulu ya White House alimesema hakuna makubaliano kama hayo bado yamefikiwa lakini inajitahidi kufikia makubaliano.

    Vita vya Gaza: Mengi zaidi

    • Je Israel inapanga kushambulia vipi mahandaki ya Hamas?Hezbollah yaonya vita vya kikanda ikiwa mashambulizi Gaza yataendelea
    • Mtoto mmoja huuawa kila baada ya dakika kumi Gaza
    • Nchi ya Amerika Kusini ambayo ina jamii kubwa zaidi ya Wapalestina nje ya Ulimwengu wa Kiarabu na Israeli
    • 'Ninapiga simu kutoka shirika la ujasusi la Israel.Tunarusha bomu, una saa mbili kuondoka’
    • Vita vya Israel na Gaza: Je, uhalifu wa kivita unatekelezwa?, sheria inasemaje?
  10. Ukraine yapigwa na 'Mawimbi' ya mashambulio ya droni za Urusi kwa usiku wa pili mfululizo

    g

    Chanzo cha picha, EPA

    Mkuu wa utawala wa mji wa Kyiv Serhiy Popko, amesema mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine iligonga takriban droni 10 katika mji mkuu Kyiv na viunga vyake.

    Hakuna "uharibifu mkubwa" au majeruhi yaliyoripotiwqa, alisema.

    Wakati huo huo, mamlaka ya Urusi ilisema ndege isiyo na rubani ya Ukraine iliyokuwa ikielekea Moscow ilidunguliwa siku ya Jumamosi.

    Wizara ya ulinzi imesema ndege hizo zisizo na rubani (UAVs) zilinaswa kwenye Wilaya ya Bogorodsky kwenye viunga vya kaskazini-mashariki mwa mji mkuu.

    Meya wa Moscow Sergei Sobyanin alisema hakuna uharibifu au majeruhi.

    Mashambulizi ya anga ya Jumapili dhidi ya maeneo yanayolengwa na Ukraine yamefuatia wimbi la mashambulio yaliyotokea usiku wa kuamkia jana, huku Kyiv ikisema kuwa imeangusha ndege 29 kati ya 38 za Shahed zilizotengenezwa na Iran zilizorushwa na Urusi.

    BBC haiwezi kuthibitisha ni ngapi ndege zisizo na rubani zilizorushwa na kuharibiwa.

    Siku ya Jumamosi, rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alilisifu jeshi lake la anga kwa kudungua UAVs - idadi kubwa zaidi ya mashambulizi ya Urusi iliyoripotiwa katika kipindi cha zaidi ya wiki sita.

    Vita vya Ukraine: Mengi zaidi:

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  11. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja ya leo Jumapili tarehe 19.11.2023