Jeshi la Israel lasema wanajeshi wake wanafanya msako katika hospitali kuu ya Gaza

Mtu aliyeshuhudia tukio hilo ndani ya hospitali anasema aliona vifaru na wanajeshi wakiingia katika idara maalumu ya upasuaji.

Moja kwa moja

  1. Avunja rekodi ya Guinness kwa kutengeneza wigi refu zaidi duniani

    .

    Chanzo cha picha, GUINESS WORLD RECORDS

    Maelezo ya picha, Helen Williams amekuwa mtengeneza wigi kwa karibu muongo mmoja

    Mwanamke mmoja raia wa Nigeria amevunja rekodi ya dunia kwa kutengeneza na kuvaa wigi refu zaidi duniani.

    Helen William alitengeneza wigi lenye urefu wa mita 351.28

    Alitumia siku 11 na dola 2500 za Marekani kutengeneza nywele hizo bandia.

    Alilazimika kutumia mafungu 1000 ya nywele, dawa za nywele 12 mirija 35 ya gundi ya nywele na vibano 6,250 vya nywele.

    "Mafanikio haya ni mojawapo ya mambo mazuri zaidi ambayo yamewahi kunitokea. Bado siwezi kuamini," alisema.

    Licha ya kuwa mtengeneza wigi kwa miaka minane, alisema haikuwa kazi rahisi kwani "alihisi kuchoka" wakati wa mchakato huo.

    "Marafiki na familia walinitia moyo. Sikutaka kuwaangusha, hivyo nilidumisha mtazamo wangu. Matokeo yake ni wigi refu zaidi lililotengenezwa kwa mkono duniani," alisema.

    Baada ya kukamilisha kipande cha nywele, kutafuta mahali pa kuiweka na kupima kwa usahihi ilikuwa vigumu. Alichagua kuweka wigi hiyo kwenye barabara kuu inayounganisha miji ya Lagos na Abeokuta tarehe 7 Julai.

    Rekodi za Dunia za Guinness zilithibitisha rekodi hiyo Jumanne.

    Bi Williams ameonyesha wigi katika ofisi yake ili watu waweze kuja na kuangalia juhudi zake za kuweka rekodi.

    Mapema mwaka huu, Hilda Baci alizua hisia nchini Nigeria alipovunja rekodi ya dunia ya kupika bila kukoma. Lakini alishindwa na raia wa Ireland Alan Fisher wiki chache zilizopita

  2. Rapa wa Nigeria Oladips afariki akiwa na umri wa miaka 28

    th

    Chanzo cha picha, oladipsoflife/Instagram

    Rapa maarufu wa Nigeria Oladipupo Oladimeji, almaarufu Oladips, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka.

    Hawakutoa sababu ya kifo chake, lakini chapisho hilo lilisema kwamba rapa huyo kwa zaidi ya miaka miwili "ameweka vita vyake ndani yake mwenyewe".

    Taarifa hiyo ilihimiza umma kuheshimu faragha ya familia yake, na kusema kwamba maelezo ya mazishi yatatangazwa baadaye.

  3. Jeshi la Israel lasema operesheni katika hospitali ya Al-Shifa bado inaendelea

    th

    Chanzo cha picha, Reuters

    Jeshi la Israel (IDF) limetoa taarifa kuhusu shughuli zake huko Gaza, likisema operesheni yake katika hospitali ya Al-Shifa inaendelea.

    IDF ilisema wanajeshi wake wanaendelea na "operesheni sahihi na inayolengwa dhidi ya Hamas katika eneo maalum katika Hospitali ya Shifa, ambapo wanafanya msako wa miundombinu na silaha za Hamas".

    Mwandishi wa habari ndani ya hospitali hiyo aliiambia BBC mapema leo asubuhi kwamba IDF ilikuwa ikienda chumba hadi chumba kuwahoji wafanyakazi na wagonjwa, wakiandamana na wakalimani na maafisa wa matibabu.

    IDF pia ilisema imepeleka msaada wa kibinadamu kwenye mlango wa hospitali.Katikataarifa ya awali, jeshi la Israeli lilisema lilikuwa linajaribu kuleta mashine za watoto wachanga na chakula cha watoto hospitalini, ambapo watoto kadhaa wanahitaji matibabu.

    Hapo awali, tulisikia kutoka kwa shirika la usaidizi ambalo lilisema hospitali tayari ina machine hizo na kinachohitajika ni mafuta ya kuwasha vifaa vya matibabu.

    Unaweza pia kusoma:

    • Hezbollah yaonya vita vya kikanda ikiwa mashambulizi Gaza yataendelea
    • Mtoto mmoja huuawa kila baada ya dakika kumi Gaza
    • Nchi ya Amerika Kusini ambayo ina jamii kubwa zaidi ya Wapalestina nje ya Ulimwengu wa Kiarabu na Israeli
    • 'Ninapiga simu kutoka shirika la ujasusi la Israel.Tunarusha bomu, una saa mbili kuondoka’
    • Vita vya Israel na Gaza: Je, uhalifu wa kivita unatekelezwa?, sheria inasemaje?
  4. Kombe la Dunia liko salama baada ya ofisi za raga za Afrika Kusini kuvamiwa na wezi

    th

    Chanzo cha picha, YOAN VALAT/EPA-EFE/REX/SHUTTERSTOCK

    Wezi wameingia katika makao makuu ya Muungano wa Rugby wa Afrika Kusini, ambapo picha za CCTV zinaonyesha wakigusa Kombe la Dunia kabla ya kuondoka.

    Wizi huo ulifanyika Jumatatu katika bustani ya ofisi katika vitongoji vya kaskazini mwa Cape Town.

    Wanaacha kombe nyuma na badala yake wanaiba Vileo, jezi tano za Springbok zilizosainiwa na kompyuta ndogo nane.

    Video hiyo inawaonyesha wanaume wakiingia kwenye chumba ambamo nakala ya kombe la William Webb Ellis imehifadhiwa.

    Katika picha ambayo imechapishwa kwenye Xna mwandishi wa habari wa Afrika Kusini Yusuf Abramjee, mmoja wa wezi anaonekana akiweka mkono wake wenye glavu kwenye kombe jingine , akiinua kidogo, kabla ya kusonga hadi kabati iliyo chini yake.

    Msemaji wa Muungano wa Raga wa Afrika Kusini aliambia BBC kwamba vikombe vyote walivyozawadiwa viko salama

    Afrika Kusini ilishinda Kombe la Dunia la Raga mnamo Oktoba 28 baada ya kuishinda New Zealand mjini Paris na kuwa taifa la kwanza kushinda mashindano hayo mara nne.

    Nchi ilisherehekea ushindi huo kwa ziara ya siku nne ya ushindi, ambapo timu ilisafiri kwa gwaride kote Afrika Kusini.

    Rais Cyril Ramaphosa, pia alitangaza tarehe 15 Disemba kama sikukuu ya umma kusherehekea mafanikio " makubwa ya Springboks".

  5. Habari za hivi punde, Mpango wa kuwahamisha hadi Rwanda wahamiaji haramu ni kinyume cha sheria, Mahakama ya Juu ya Uingereza yaamuru

    TH

    Chanzo cha picha, PA Media

    Mpango wa serikali ya Uingereza kuwapeleka wahamiaji haramu Rwanda ni kinyume na sheria , imesema mahakama ya Juu nchini Uingereza.Lord Reed ameamuru kwamba kulikuwa na sababu kubwa za kuamini kwamba wakimbizi wa kweli waliotumwa nchini humo wanaweza kuwa katika hatari ya kurudishwa katika nchi walizokimbia.

    Kwa hivyo rufaa ya katibu wa nyumba inatupiliwa mbali, Lord Reed anasema.

    "Jaribio la kisheria ambalo linapaswa kutumika katika kesi hii ni kama kuna sababu kubwa za kuamini kwamba wanaotafuta hifadhi waliotumwa Rwanda watakuwa katika hatari ya kurudishwa tena [hii ina maana kuwarudisha watu katika nchi zao].

    "Kwa mujibu wa ushahidi nilionao, Mahakama ya Rufaa iliamuru kuwa kulikuwa na sababu hizo. Tuna maoni kwa kauli moja kwamba walikuwa na haki ya kufikia uamuzi huo. Hakika, baada ya kuchukuliwa kwa ushahidi wenyewe, tunakubaliana na uamuzi huo

    “Tunakubali maoni ya katibu wa mambo ya ndani kwamba serikali ya Rwanda iliingia mkataba huo kwa nia njema, na kwamba uwezo wa mfumo wa Rwanda wa kutoa maamuzi sahihi na ya haki unaweza kujengeka na utajengeka.

    "Walakini, tukijiuliza kama kulikuwa na sababu kubwa za kuamini kuwa hatari ya kweli ya kufutwa tena ilikuwepo wakati huo huo, tumehitimisha kuwa kulikuwa na.

    "Mabadiliko yanayohitajika ili kuondoa hatari ya kurudishwa tena yanaweza kutolewa katika siku zijazo, lakinihayajaonyeshwa kuwa yapo sasa.

    Serikali ya Rwanda: Tun mashaka na uamuzi huu

    Dakika chache baada ya uamuzi huo, serikali ya Rwanda imetoa tamko hili, ikisema "haijafurahia " kutajwa kama eneo ambalo sio nchi ya tatu salama.

    Hii hapa taarifa kamili:

    "Hatimaye huu ni uamuzi wa mfumo wa mahakama wa Uingereza.

    "Hata hivyo, tunapingana na uamuzi kwamba Rwanda sio nchi ya tatu salama kwa wanaotafuta hifadhi na wakimbizi. Rwanda na Uingereza zimekuwa zikifanya kazi pamoja ili kuhakikisha kuunganishwa kwa waomba hifadhi waliohamishwa katika jamii ya Rwanda.

    "Rwanda imejitolea kutekeleza majukumu yake ya kimataifa, na tumetambuliwa na UNHCR na taasisi nyingine za kimataifa kwa jinsi tunavyowashughulikia wakimbizi.

    "Katika mchakato huu wa kisheria tumekuwa na shughuli nyingi kuendelea kutoa maendeleo kwa Wanyarwanda, na kufanya kazi pamoja na washirika wa kimataifa kutatua baadhi ya changamoto kubwa ambazo Afrika na dunia nzima inakabiliana nazo.

    "Tunachukua majukumu yetu ya kibinadamu kwa uzito, na tutaendelea kuyatekeleza'

    Sunak 'anashughulikia' mkataba mpya na Rwanda

    th

    Chanzo cha picha, PA Media

    Waziri Mkuu Rishi Sunak ameliambia bunge la Commons kwamba "atakamilisha" mkataba mpya na Rwanda kwa kuzingatia uamuzi wa Mahakama ya Juu.

    Anaongeza kuwa "yuko tayari kurekebisha mifumo yetu ya kisheria ya ndani" ikiwa ni lazima.

    "Serikali imekuwa ikifanya kazi tayari juu ya mkataba mpya na Rwanda na tutakamilisha hilo kutokana na uamuzi wa leo," anasema.

    "Zaidi ya hayo, ikibidi niko tayari kurekebisha mifumo yetu ya kisheria ya ndani."

    Anasema iwapo itabainika kuwa “mifumo yetu ya ndani ya sheria au mikataba ya kimataifa” inakatisha mipango yetu basi “niko tayari kubadili sheria zetu na kupitia upya mahusiano hayo ya kimataifa”.

    "Watu wa Uingereza wanatarajia tufanye chochote kinachohitajika kusimamisha boti na hilo ndilo ambalo serikali hii itatoa."

  6. Wanajeshi wa Israel wanawahoji watu katika hospitali ya Al-Shifa- shuhuda,

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Nimezungumza na shahidi aliyeshuhudia hali ya mambo ndani ya hospitali ya Al-Shifa. Hiki ndicho alichoniambia kuhusu uvamizi wa Jeshi la Ulinzi la Israel kwenye kituo hicho.

    Khader, mwandishi wa habari ambaye yuko hospitalini, anasema vikosi vya Israeli vinaenda chumba hadi chumba, sakafu kwa sakafu kuhoji kila mtu - wafanyakazi na wagonjwa - na wanaandamana na madaktari huku wakizungumza kwa Kiarabu.

    Watu waliokimbia makazi yao ambao wamepata hifadhi katika hospitali hiyo wamekusanyika ndani ya uwanja wa hospitali na baadhi wanakaguliwa na maafisa wa usalama.

    Anaongeza kuwa jeshi la Israel liko katika "udhibiti kamili" na hakuna ufyatuaji risasi unaofanyika.

    BBC haijaweza kuthibitisha madai kwamba wanajeshi wa Israel sasa wanadhibiti hospitali ya Al-Shifa. Hapo awali, jeshi la Israeli lilisema lilikuwa likifanya "operesheni sahihi " katika eneo maalum la hospitali.

    Shuhuda huyo kwa jina Khader aliniambia kuwa kwa kutumia vipaza sauti, askari wa IDF wamewataka wanaume wote wenye umri wa kati ya miaka 16 hadi 40 kuondoka ndani ya majengo ya hospitali, isipokuwa idara za upasuaji na dharura, na kwenda kwenye uwanja wa hospitali.

    Saa moja iliyopita, alisema askari walifyatua risasi hewani kuwalazimisha waliobaki ndani kutoka nje.

    Pia alisema wamefunga kifaa cha uchunguzi wa skani (scan).

    BBC haijaweza kuthibitisha madai hayo kwa uhuru.

    Unaweza pia kusoma:

    • Hezbollah yaonya vita vya kikanda ikiwa mashambulizi Gaza yataendelea
    • Mtoto mmoja huuawa kila baada ya dakika kumi Gaza
    • Nchi ya Amerika Kusini ambayo ina jamii kubwa zaidi ya Wapalestina nje ya Ulimwengu wa Kiarabu na Israeli
    • 'Ninapiga simu kutoka shirika la ujasusi la Israel.Tunarusha bomu, una saa mbili kuondoka’
    • Vita vya Israel na Gaza: Je, uhalifu wa kivita unatekelezwa?, sheria inasemaje?
  7. Vita vya Israel-Gaza: Marekani yathibitisha Hamas inaendesha harakati za kijeshi katika chumba cha chini cha Hospitali ya Al-Shifa

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Maelfu ya watu wanaaminika kuwa wamejihifadhi katika hospitali ya Al Shifa.

    Marekani imesema ina habari kwamba Hamas ilikuwa ikiendesha kituo cha amri na udhibiti wa kijeshi katika chumba cha chini cha hospitali ya Al-Shifa katika mji wa Gaza.

    John Kirby, mratibu wa kimkakati wa mawasiliano wa Baraza la Usalama la Kitaifa la Marekani, amesema Hamas huhifadhi silaha katika vyumba vya chini vya hospitali na hujitayarisha kwa shambulio la Israeli.

    Hii ni mara ya kwanza kwa mshirika wake, Marekani, kuunga mkono kwa uhuru madai ya Israel kwamba Hamas ina kambi ya kijeshi iliyofichwa katika hospitali hiyo. Hamas inakanusha madai haya.

    Tangazo hilo linakuja huku Israel ikikabiliwa na shinikizo kutoka kwa jumuiya ya kimataifa kuwalinda raia waliokwama hospitalini.

    Hapo awali, Rais wa Marekani Joe Biden alisema Hospitali ya Al Shifa "lazima ilindwe" kutokana na mapigano makali yanayoizunguka, huku Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak akisema Israel lazima ichukue hatua kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

    Eneo linalozunguka Hospitali ya Al Shifa, kubwa zaidi huko Gaza, limekuwa kitovu cha mapigano katika siku za hivi karibuni. Maelfu ya watu wanaaminika kuwa wamejihifadhi katika hospitali ya Al Shifa.

    Unaweza pia kusoma:

    • Hezbollah yaonya vita vya kikanda ikiwa mashambulizi Gaza yataendelea
    • Mtoto mmoja huuawa kila baada ya dakika kumi Gaza
    • Nchi ya Amerika Kusini ambayo ina jamii kubwa zaidi ya Wapalestina nje ya Ulimwengu wa Kiarabu na Israeli
    • 'Ninapiga simu kutoka shirika la ujasusi la Israel.Tunarusha bomu, una saa mbili kuondoka’
    • Vita vya Israel na Gaza: Je, uhalifu wa kivita unatekelezwa?, sheria inasemaje?
  8. Vita vya Gaza: Hamas inasema uvamizi wa Al-Shifa ni 'uhalifu dhidi ya binadamu'

    g
    Maelezo ya picha, Kiongozi wa Hamas Khaled Meshaal

    Ofisi ya habari vya serikali ya Hamas imetoa taarifa ikiutaja uvamizi wa Israel katika hospitali ya Al-Shifa ya Gaza kuwa ni "uhalifu wa kivita", "uhalifu wa kimaadili" na "uhalifu dhidi ya binadamu".

    Ilisema wagonjwa 9,000, wahudumu wa afya na raia walioyakimbia makazi yao walikuwa hospitalini wakati uvamizi huo uliofanyika usiku.

    Katika video kwenye X, (zamani ikiitwa Twitter,) na Kituo cha Habari cha Palestina, kiongozi wa Hamas Izzat al-Rishq alisema Israeli ilishambulia kituo cha kiraia, sio eneo la kijeshi.

    Katika taarifa ya awali, Hamas ilisema inaiwajibuisha Washington na rais wa Marekani Joe Biden kuhusika na uvamizi huo.

    Israel na Marekani zinadai kuwa Hamas - kundi la kigaidi lililopigwa marufuku nchini Marekani, Uingereza na EU - lina kambi yake chini ya hospitali kuu ya Al-Shifa, jambo ambalo Hamas inakanusha.

  9. Mshukiwa aliyesakwa sana kwa mauaji ya kimbari ya Rwanda alifariki miaka 25 iliyopita - UN,

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Shirika la Umoja wa Mataifa linathibitisha kuwa Aloys Ndimbati (katikati) alifariki mwaka 1997

    Umoja wa Mataifa umethibitisha kifo cha Aloys Ndimbati, mtuhumiwa mauji ya ki aliyesakwa sanakwa uhalifu wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 alifariki miaka 25 iliyopita.

    Katika taarifa yake, kitengokinachoshughulikia kesi zilizoachwa na Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda mjini Arusha (ICTR), kinasema kuwa Aloys Ndimbati alifariki dunia mwishoni mwa Juni mwaka 1997.

    Kitengo hichokinasema kwamba ilichukua miaka hiyo yote ya mashauri kabla ya kufikia uamuzi kuwa alifariki.

    Ndimbati alishtakiwa kwa makosa saba ya mauaji ya halaiki, uhalifu ambao inasemekana aliufanya katika manispaa ya Gisovu, ambako alikuwa mbabe wakati wa mauaji ya kimbari.

    Kulingana na kitengo hicho , Ndimbati alifariki mwishoni mwa Juni mwaka 1997,katikakijiji chaGatore katika wilaya ya Kirehe jimbo la Mashariki mwa Rwanda.

    Taarifa Zaidi zinasema kwamba alikuwa amerejea mwezi Junimwaka 1997 kutoka Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo), ambako alikuwa amekimbia na familia yakemwezi Julai ,1994, baada ya mauaji ya kimbari.

    Hata hivyo, tangu alipowasili katika kijiji cha Gatore, hakuna taarifa zozote kumhusu zilizojulikana, isipokuwa uchunguzi wa Umoja wa Mataifa unathibitisha kwamba hakuondokamahali hapo.

    Kutokana na hali yamtafaruku uliokuwepo wakati huo, taarifa hiyo inasema kuwa haikufahamika ni kwa namna gani Aloys Ndimbati alifariki.

    Shirika la Umoja wa Mataifa, hata hivyo, linasema kuwa kifo hicho kimethibitishwa na ofisi ya mashtaka ya Rwanda katika uchunguzi wake.

    Wakati wa mauaji ya kimbari, Aloys Ndimbati alikuwa mkuu wa wilaya ya Gisovu katika mkoa wa zamani wa Kibuye. Hapo ndipo inasemekana aliamuru mauaji ya Watutsi.

  10. Israel 'inafanya kila tuwezalo kulivunja kundi la Hamas': Naibu Balozi wa Marekani

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Israel inawashutumu Hamas kwa kuwatumia watu ndani ya hospitali ya Al Shifa kama ngao ya vita

    Naibu balozi wa Israel mjini New York amezungumza na BBC kuhusu operesheni ya sasa ya kijeshi katika eneo la Al-Shifa.

    Tsach Saar aliulizwa ni nini hasa kilichosababisha "operesheni ya makusudi na inayolengwa katika Al-Shifa dhidi ya Hamas" inamaanisha.

    "Ina maana kwamba tunafanya kila tuwezalo ili kuvunja uwezo wa Hamas," alisema, akiongeza kuwa Hamas "iliweka wapiganaji wake na silaha ndani na Hospitali ya Shifa. Na hawakutumia njia hiyo kwenye hospitali pekee.

    "Kila kitu tunachoweza kumaanisha kwamba tunachukua silaha, kwamba tunavunja uwezo wa wapiganaji wao, magaidi wao, wakati tukihakikisha kwamba tunapunguza uharibifu wa dhamana, kupoteza maisha ya raia wasio na hatia. Hii ndiyo maana yake."

    Pia aliulizwa ikiwa Israel ilifanya juhudi za kuwaondoa wagonjwa hospitalini mapema.

    "Tunachukua kila hatua ambayo inawezekana," alisema Bwana Saar.

    "Kuwezesha a wagonjwa na watu, watu wasio na hatia ambao wako hospitalini kuhakikisha kuwa wanaondoka salama. Lakini kwa bahati mbaya, Hamas hutumia `binadamu kama ngao zao , kuwazuia kutoka hospitali hii kwa sababu wanajua kwamba wanawalinda kwa uwepo wao huko."

    Matamshi yake yanakuja wakati Marekani imesema ina taarifa zake za kiintelijensia kwamba Hamas ina kituo cha udhibiti na udhibiti chini ya Al-Shifa - madai ambayo Hamas imekuwa ikiyakanusha.

    Unaweza pia kusoma:

    • Hezbollah yaonya vita vya kikanda ikiwa mashambulizi Gaza yataendelea
    • Mtoto mmoja huuawa kila baada ya dakika kumi Gaza
    • Nchi ya Amerika Kusini ambayo ina jamii kubwa zaidi ya Wapalestina nje ya Ulimwengu wa Kiarabu na Israeli
    • 'Ninapiga simu kutoka shirika la ujasusi la Israel.Tunarusha bomu, una saa mbili kuondoka’
    • Vita vya Israel na Gaza: Je, uhalifu wa kivita unatekelezwa?, sheria inasemaje?
  11. 'Hatutaki kuona makabiliano ndani ya hospitali'- Marekani

    Taarifa kutoka Ikulu ya Marekani zinasema Rais Joe Biden na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wamejadiliana kwa njia ya simu.

    Katika taarifa, White House ilisema viongozi hao "walijadili kwa kina juhudi zinazoendelea za kuwaokoa mateka wanaouzuiliwa na Hamas, ikiwa ni pamoja na watoto na baadhi ya raia wa Marekani".

    Wakati huo huo Ikulu ya Marekani imetoa kauli ya kwanza kuhusu uvamizi wa Israel dhidi ya hospitali ya Al-Shifa mjini Gaza.

    "Hatuungi mkono mapigano ndani ya hospitali na hatutaki kuona milipuko ya moto katika hospitali ambayo ina watu wasio na hatia, watu wasiojiweza, wagonjwa wanaojaribu kupata matibabu na wasiostahili kukumbwa na mapigano," msemaji aliambua Baraza la Usalama la Kitaifa la White House.

    Alikariri msimamo wa Rais Biden wa mapema Jumanne kwamba hospitali na wagonjwa lazima walindwe.

  12. Je, ni watu wangapi wamo ndani yahospitali iliyozingirwa ya Al-Shifa?

    G

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelfu ya wagonjwa na raia wanaaminika kupata hifadhi katika hospitali ya Al-Shifa ya Gaza, ambayo imezingirwa na wanajeshi wa Israel.

    Hata makadirio hivyo yanatofautiana. Shirika la Afya Duniani (WHO) mapema Jumanne lilisema kulikuwa na wagonjwa wapatao 700, wafanyikazi 400 wa hospitali na raia 3,000 ka ndani ya Al-Shifa.

    Wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas imesema kuna angalau watu 2,300 ambao bado wamo ndani ya hospitali – wagonjwa wapatao 650, wafanyakazi 200-500 na karibu raia 1,500.

    Unaweza pia kusoma:

    • Hezbollah yaonya vita vya kikanda ikiwa mashambulizi Gaza yataendelea
    • Mtoto mmoja huuawa kila baada ya dakika kumi Gaza
    • Nchi ya Amerika Kusini ambayo ina jamii kubwa zaidi ya Wapalestina nje ya Ulimwengu wa Kiarabu na Israeli
    • 'Ninapiga simu kutoka shirika la ujasusi la Israel.Tunarusha bomu, una saa mbili kuondoka’
    • Vita vya Israel na Gaza: Je, uhalifu wa kivita unatekelezwa?, sheria inasemaje?
  13. Wanajeshi wa Israel 'wavamia' hospitali kuu ya Gaza

    XX

    Chanzo cha picha, AFP

    Jeshi la Israel limefanya operesheni dhidi ya Hamas iliyolenga moja kwa moja hospitali ya Al Shifa mjini Gaza. Jeshi hilo limetaka kujisalimisha kwa watu linaowaita magaidi.

    Mtu aliyekuwa ndani ya hospitali ya Al-Shifa amemwambia mwandishi wa BBC Rushdi Abu Alouf kwamba a wanajeshi wa Israel wameanza kuivamia.

    "Askari walirusha bomu la machozi ambalo lilisababisha watu kukosa hewa," anasema Khader Al-Zaanoun.

    "Niliona wanajeshi wakiingia katika idara maalumu ya upasuaji," Khader aliniambia kabla ya mawasiliano naye kukatika, anasema Rushdi.

    Hii ni mara ya kwanza kwa wanajeshi wa Isarel wameingia ndani ya hospitali ya Al-Shifa baada ya siku kadhaa za mashambulizi na mapigano makali huko Gaza.

    Awali,msemaji wa idara ya afya Gaza Ashraf al Qidra aliwaomba viongozi wa Misri,Qatar na Umoja wa Mataifa kuingilia kati kuokoa maisha ya wagonjwa na wafanyakazi walioko ndani ya hospitali hiyo.

    Al-Shifa ndiyo hospitali kubwa zaidi huko Gaza, na Israel na Marekani zinadai kuwa Hamas ina kambi yake kuu - ambayo Hamas inakanusha.

    BBC haijafanikiwa kuthibitisha madai hayo ya Israel na Marekani.

    Wafanyakazi wa misaada wanasema hali ndani ya Al-Shifa ni "mbaya" na wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas inasema kuna maelfu ya watu wanaotumia eneo hilo kujikinga dhidi ya mashambulizi ya Israel.

    Kituo hicho pia kinaishiwa na mafuta, maafisa wanasema, jambo ambalo limefanya kuwa vigumu kwa wafanyikazi kusaidia wagonjwa wanaohitaji huduma ya dharura - ikiwa ni pamoja na watoto wanaozaliwa kabla ya wakati ambao wametolewa kwenye vyumba maalum kutokana na kukatika kwa umeme, madaktari wanasema.

    Hapo awali, daktari mmoja aliambia BBC kwamba takriban watu 200 wamezikwa katika kaburi la pamoja huko Al-Shifa, baada ya maiti zilizoharibika zilizorundikana katika hospitali hiyo.

    Unaweza pia kusoma:

    • Hezbollah yaonya vita vya kikanda ikiwa mashambulizi Gaza yataendelea
    • Mtoto mmoja huuawa kila baada ya dakika kumi Gaza
    • Nchi ya Amerika Kusini ambayo ina jamii kubwa zaidi ya Wapalestina nje ya Ulimwengu wa Kiarabu na Israeli
    • 'Ninapiga simu kutoka shirika la ujasusi la Israel.Tunarusha bomu, una saa mbili kuondoka’
    • Vita vya Israel na Gaza: Je, uhalifu wa kivita unatekelezwa?, sheria inasemaje?
  14. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Jumatano 15.11.2023

    xx

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Ikiwa ndio mwanzo unajiunga nasi ufuatao ni mukhtasari wa habari za dunia:

    • Jeshi la Israel limefanya operesheni dhidi ya Hamas iliyolenga moja kwa moja hospitali ya Al Shifa mjini Gaza. Jeshi hilo limetaka kujisalimisha kwa watu linowaita magaidi.
    • Kundi la Hamas limejibu hatua hiyo kwa kuelekeza kidole cha lawama wa Rais Joe Biden wa Marekani.
    • Hali ya tahadhari imetangazwa karibu kote nchini Brazil ambako kunashuhudiwa ongezeko kubwa la viwango vya joto.
    • Bunge la Marekani limepitisha mswada wa muda wa matumizi ya fedha ili kuepusha shughuli za serikali kusitishwa.
    • Rais wa China, Xi Jinping,amewasili San Francisco kwa ajili ya mazungumzo baadae leo na Rais Joe Biden. Mkutano huo utakuwa wa kwanza kati ya viongozi hao wawili katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
    • Na Marekani itaanza kutoa tena misaada ya chakula kote Ethiopia kuanzia mwezi ujao Desemba,miezi sita tangu kusitisha misaada hiyo.