Vita vya Ukraine 'kutakuwa na maeneo mapya zaidi ndani ya Urusi'- Medvedev
Naibu mkuu wa Baraza la usalama la Urusi Dmitry Medvedev alisema kwamba idadi ya kile kinachoitwa "maeneo mapya" ya Urusi itaongezeka katika siku zijazo.
Moja kwa moja
Majeruhi wa Ligi Kuu - 'Wachezaji hawawezi tena kukabiliana na mzigo huu uliokithiri'

"Wachezaji hawawezi tena kukabiliana na mzigo huu."
Hayo ni maneno ya kusikitisha ya Erik ten Hag wakati meneja wa Manchester United akipambana na orodha inayoongezeka ya majeruhi.
Mholanzi huyo alikuwa akizungumza siku ambayo mlinzi wake Lisandro Martinez alitolewa nje hadi mwisho wa mwisho , na hivyo kufanya jumla ya wachezaji wasiokuwepo United kufikia wanane.
Lakini Ten Hag sio meneja pekee wa Premier League ambaye atakabiliwa na orodha ndefu ya majeruhi wiki sita tu baada ya msimu mpya.
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anafikiri wachezaji wanapaswa kukusanyika ili kulazimisha mabadiliko ya ratiba.
Meneja wa Newcastle Eddie Howe, meneja wa Arsenal Mikel Arteta na mkufunzi wa Chelsea Mauricio Pochettino pia wamekuwa na maoni yao kuhusu suala hilo.
Kulingana na PremierInjuries.com, Timu 20 za Ligi kuu za Uingereza kwa sasa zina jumla ya wachezaji 112 ambao wamejeruhiwa.
Nagorno-Karabakh: Armenia inasema wakimbizi 100,000 wanakimbia

Chanzo cha picha, AFP VIA GETTY IMAGES
Zaidi ya watu 100,000 wamekimbia eneo la Nagorno-Karabakh, Armenia inasema.
Hii inamaanisha kwamba karibu wakazi wote wa kabila la Armenia wameondoka tangu Azerbaijan ilipotwaa eneo hilo wiki iliyopita.
Azerbaijan imesema inataka kuunganisha eneo hilo na kuwachukulia wakaazi wake sawa, lakini msemaji wa Armenia alisema huu ni "uongo".
Nagorno-Karabakh - inayotambuliwa kama sehemu ya Azerbaijan - ilikuwa inaendeshwa na Waarmenia wa kabila kwa miongo mitatu.
Eneo la milima katika Caucasus Kusini limeungwa mkono na Armenia - lakini pia na mshirika wake, Urusi.
Takriban Waarmenia 200 wa kabila na makumi ya wanajeshi wa Azerbaijan waliuawa wakati jeshi la Azerbaijan likiingia ndani.
Kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano, wanaotaka kujitenga wamekubali kusalimisha silaha zao.
Kampuni ya Uturuki yawekeza dola milioni 100 katika uzalishaji wa ndege zisizo na rubani nchini Ukraine

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Mwaka 2022, wakaazi wa Kilithuania walichangisha pesa kwa ajili ya kuipeleka ndege isiyo na rubani ya Bayraktar TB-2 kama msaada kwa jeshi la Ukraine Kampuni ya Uturuki ya Baykar, inayotengeneza ndege zisizo na rubani za Bayraktar TB-2, itawekeza dola milioni 100 katika uzalishaji wa ndege hizo nchini Ukraine, mkuu wake Haluk Bayraktar alisema katika kongamano mjini Kiev.
Kiwanda cha kutengeneza ndege zisizo na rubani za Uturuki kitajengwa baada ya mwaka mmoja na nusu na kitaajiri watu 300, mfanyabiashara huyo alisema.
Katika Ukraine, kulingana na yeye, pia kuna kituo cha huduma kwa ajili ya huduma hiyo, pamoja na ofisi ya kampuni.
Makubaliano ya utengenezaji wa ndege hizo nchini Ukraine yalipitishwa hata kabla ya kuanza kwa uvamizi kamili wa Urusi. Mapema mwezi Februari 2022, yalitiwa saini na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na kiongozi wa Ukraine Vladimir Zelensky.
Mamlaka ya Uturuki ilitoa leseni kwa Baykar kutengeneza ndege zisizo na rubani nchini Ukraine mnamo Juni 2023.
Inakuwezesha kuandaa mzunguko kamili wa uzalishaji wa aina mbili za droni za mashambulizi ya kupambana za aina ya - Bayraktar TB2 na Bayraktar Akinci.
Mnamo mwaka wa 2019, Baykar ilianzisha kampuni ya Avia Ventures LLC huko Ukraine - inatarajiwa kwamba biashara hii, kwa niaba ya Baykar, itahusika katika ujenzi wa kiwanda cha utengenezaji wa ndege zisizo na rubani.
Ndege zisizo na rubani zitakazotengenezwa nchini Ukraine zitakuwa na injini zinazotengenezwa na Ukraine.
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Mwanamume afariki nchini Australia baada ya nyangumi kugonga boti

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Ufuo wa Australia una aina 10 kubwa na 20 ndogo za nyangumi Nyangumi mmoja ameigonga mashua nchini Australia na kumuua mtu mmoja na kumwacha mwingine kujeruhiwa, polisi wamesema.
Watu hao walikuwa kwenye msafara wa uvuvi wakati mashua yao ilipogongwa na maji karibu na La Perouse, kilomita 14 (maili tisa) kusini-mashariki mwa Sydney.
Maafisa waligundua kuwa kuna hali ya tahadhari ilipandishwa baada ya chombo kuonekana bila mtu yeyote na kuzunguka.
Vifo vinavyosababishwa na nyangumi katika eneo hilo ni nadra, na waziri wa serikali wa New South Wales aliiita "ajali mbaya kabisa".
Polisi walisema katika taarifa kwamba uwezekano wa mgongano ulisababisha mashua kuinama, na kuwatupa watu wote baharini.
"Taarifa za mapema ni kwamba nyangumi anaweza kuvunja karibu na boti, au kwenye mashua," Kaimu Mratibu wa Polisi wa Maji Siobhan Munro alisema, akiongeza kuwa hajawahi kuona tukio kama hilo hapo awali.
Muathiriwa, 61, alipatikana akiwa amepoteza fahamu na alifariki katika eneo la tukio, maafisa walisema.
Vita vya Ukraine 'kutakuwa na maeneo mapya zaidi ndani ya Urusi'- Medvedev

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Dmitry Medvedev Naibu mkuu wa Baraza la usalama la Urusi Dmitry Medvedev alisema kwamba idadi ya kile kinachoitwa "maeneo mapya" ya Urusi itaongezeka katika siku zijazo.
Medvedev alichapisha taarifa kwenye telegramu yake katika hafla ya "Siku ya Kuunganishwa tena kwa Mikoa Mpya na Urusi" – siku hiyo ya mapumziko ilitangazwa hivi karibuni na amri ya Vladimir Putin na inaadhimishwa mnamo Septemba 30.
Aliahidi kwamba "operesheni maalum ya kijeshi itaendelea hadi uharibifu kamili wa utawala wa Nazi wa Kyiv na ukombozi wa maeneo ya awali ya Urusi yatoke kwa adui. ”
"Na kutakuwa na maeneo mapya zaidi ndani ya Urusi," Medvedev alihitimisha kauli yake.
Mnamo Septemba 30, 2022, viongozi wa Urusi walikamilisha mchakato huo, ambao waliita kuingia Shirikisho la Urusi la mikoa minne ya Ukraine, na Kyiv na nchi nyingi za ulimwengu zinalitaja jaribio hilo kuwa haramu la unyakuzi.
Uamuzi wa Urusi wa kujumuisha mikoa minne ya Ukraine (Mikoa ya Donetsk, Luhansk, Kherson na Zaporozhye) hautambuliwi na nchi nyingi, na pia ulilaaniwa na uamuzi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Jeshi la Urusi halidhibiti kabisa lolote la mikoa minne ya Kiukreni, ikiwa ni pamoja na miji ya Kherson na Zaporozhye.
Kyiv anasisitiza kuwa mazungumzo ya amani na Urusi yanaweza kuanza tu baada ya jeshi la Urusi kuondolewa kabisa katika eneo linalotambulika kimataifa kuwa la Ukraine, ikiwemo Crimea.
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Vatcan: Makardinali wapya 21 wasimikwa wakiwemo 3 kutoka Afrika

Chanzo cha picha, Vatcan News
Viongozi wa Kikatoliki cheo cha Makardinali 21 wamesimikwa hii leo na Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis.
Makardinali wapya hao wamesimikwa rasmi katika mkutano wa kawaida wa Baraza la Makardinali unaofanyika Jumamosi Septemba 30 mjini Vatican.
Mnamo tarehe 9 Julai 2023 Baba Mtakatifu Francis aliwateua Makardinali wapya 21 kati yao Makardinali watatu wakiwa ni kutoka bara la Afrika ambao ni Askofu mkuu mwandamizi Protase Rugambwa wa Jimbo kuu la Tabora, Tanzania, Askofu mkuu Stephen Ameyu Martin MULLA, Jimbo kuu la Juba, Sudan ya Kusini pamoja na Askofu mkuu Stephen Brislin wa Jimbo kuu la Cape Town, Afrika Kusini.
Makardinali wapya wataingizwa kwenye Jimbo kuu la Roma kama ishara ya kuonesha Mshikamano na Umoja na Khalifa wa Mtakatifu Petro na Makanisa mahalia yaliyoenea kila kona ya dunia.
Tanzania Baba Mtakatifu Francisko alimteuwa Askofu mkuu Protase Rugambwa mnamo tarehe 13 Aprili 2023 kuwa Askofu mkuu mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Tabora, Tanzania.
Awali alikuwa ni Katibu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu, huduma aliyobobea kwa miaka mingi kuanzia mwaka 2002 hadi mwaka 2008

Chanzo cha picha, Vatcan News
Tanzania Baba Mtakatifu Francisko alimteuwa Askofu mkuu Protase Rugambwa mnamo tarehe 13 Aprili 2023 kuwa Askofu mkuu mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Tabora, Tanzania.
Awali alikuwa ni Katibu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu, huduma aliyobobea kwa miaka mingi kuanzia mwaka 2002 hadi mwaka 2008
Tazama: Tukio la mauaji ya Tupac
Maelezo ya video, Tazama: picha kutoka hifadhi ya kumbukumbu za picha kutoka tukio la mauaji ya Tupac Picha za kumbukumbu zinaonyesha tukio la mauaji ya Tupac.
Mwimbaji huyo wa muziki wa hip-hop alipigwa risasi akiwa kwenye gari Las Vegas Marekani mwaka 1996.
Wanajeshi wa kike wa Israel wapigwa marufuku kama walinzi baada ya madai ya kushiriki ngono na mfungwa wa Kipalestina

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Waziri wa Usalama wa Taifa wa Israel Itamar Ben-Gvir alisema wanajeshi wa kike watapigwa marufuku kuwa walinzi katika magereza yenye ulinzi mkali. Wanajeshi wa kike wa Israel watapigwa marufuku kuhudumu kama walinzi wa magereza baada ya tuhuma za kufanya mapenzi na mfungwa wa Kipalestina.
Vyombo vya habari vya Israel vinasema mwanajeshi alikiri kuwa na urafiki wa kimwili na mwanamume wa Kipalestina anayesemekana kufanya shambulio baya dhidi ya raia wa Israel.
Mwanamke huyo anafikiriwa kuwa katika huduma ya kijeshi ambayo ni lazima kwa Waisraeli wengi.
Wanawake lazima wahudumu kwa angalau miaka miwili na wanaume kwa miezi 32.
Jina la askari na mfungwa anayetumikia kifungo cha maisha halijatolewa.
Mahakama inayosikiliza kesi hiyo iliamuru maelezo mengine yakiwemo eneo la gereza hilo yasifichuliwe.
Vyombo vya habari vya Israel pia viliripoti kwamba wakati wa kuhojiwa, askari huyo - ambaye amekamatwa - alidai wanawake wengine wanne pia walikuwa na uhusiano wa karibu na mwanamume huyo.
Watu sita wamefariki huku 15 wengine wakikwama baada ya mgodi wa dhahabu kuporomoka Zimbabwe

Chanzo cha picha, ANADOLU AGENCY
Maelezo ya picha, Maelfu ya wachimbaji madini kote barani Afrika wanahatarisha maisha yao wakitafuta dhahabu Watu sita wamefariki na wengine 15 wamenaswa, baada ya mgodi wa dhahabu kuporomaka nchini Zimbabwe, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.
Watu zaidi ya 30 walikwama kufuatia kuporomoka kwa mgodi wa dhahabu wa Bay Horse uliopo Chegutu, kilomita 100 (maili 62) magharibi mwa mji mkuu Harare siku ya Ijumaa asubuhi.
Wachimba migodi kumi na watatu wanasemekana kutoroka au kuokolewa.
Juhudi za kuwapata wale waliosalia chini ya ardhi zinaendelea, kituo cha televisheni cha ZBC kiliripoti.
Haijulikani ni nini kilisababisha kuanguka.
Shirikisho la Wachimbaji Madini la Zimbabwe lilisema katibu mkuu wake na mwenyekiti wa Chama cha Wachimba Madini wa Chegutu watakwenda kwenye eneo hilo kujaribu kubaini kilichotokea.
Ajali za uchimbaji madini nchini Zimbabwe - ambayo ina akiba kubwa ya dhahabu, platinamu na almasi - si za kawaida.
Mbinu za uchimbaji madini mara nyingi ni za viwango vya chini huku usalama ukipuuzwa kwa kiasi kikubwa.
Mnamo mwaka wa 2019, wachimbaji kadhaa walikufa majibaada ya mvua kubwa kunyesha mafuriko kwenye migodi ya Silver Moon na Cricket karibu na mji wa Kadoma katikati mwa nchi.
Unaweza pia kusoma:
- Watu wanne wahofiwa kufa baada ya kunaswa chini ya mgodi Afrika Kusini
- Watu wanne wahofiwa kufa baada ya kunaswa chini ya mgodi Afrika Kusini
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara ya leo Jumamosi tarehe 30.09.2023

